Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Mkaundi Maaalum Dkt. John Jingu, tarehe 24 Oktoba, 2025 amegawa pikipiki nane (8) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa ngazi ya kata mkoani Njombe huku akiwataka Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoani Njombe kutunza na kutumia kwa umakini pikipiki walizopewa na Serikali kwa ajili ya kuboresha utendaji na utoaji huduma kwa wananchi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju tarehe 24 Oktoba 2024 amekabidhi pikipiki nane (8) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Geita kutpka Kata za Muganza, Kigongo, Lwamgasa, Shabaka, Uyovu, Namonge, Masumbwe na Lulembela katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa huo.
Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju akikabidhi pikipiki Leo tarehe 24 Oktoba 2025 kwa maafisa maendeleo ya jamii katika Mkoa wa Kagera na kusema maendeleo ya kweli yapo kwa wananchi, hivyo ni muhimu watumishi hao kuwafikia hadi ngazi za vijiji.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Felister Mdemu akimkabidhi kofia ngumu ya pikipiki Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Daudi Sebyiga kamaishara ya kumkabidhi pikipiki nane (8) kwa Halmashauri nne za Mkoa wa Rukwa kwa ajili ya Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Kata tarehe 24 Oktoba, 2025, hatua inayolenga kuwawezesha maafisa hao kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi katika kuwahudumia wananchi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Felister Mdemu ( wa pili kulia), amekabidhi pikipiki nane (8) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri nne (4) mkoani Songwe tarehe 23 Oktoba, 2025 huku akiwataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na kujituma zaidi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu tarehe 22 Oktoba, 2025 akikabidhi pikipiki kumi (10) kwa Maofisa Mendeleo ya Jamii Mkoani Iringa.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Felister Mdemu tarehe 22 Oktoba, 2025 amekabidhi Pikipiki kumi na mbili (12) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii katika hafla fupi iliyofanyika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya lengo kuu ikiwa ni kuwasaidia Maafisa hao hasa wanaoishi vijijini kuzitumia kuwafikia wananchi na kuwahudumia kwa wakati.
Baadhi ya waananchi waliowezeshwa mafunzJamiio ya ushonaji katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Felister Mdemu alipotembeea kukagua uendeshaji wa miradi Chuoni hapo Oktoba 17,2025 Mkoani Iringa.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu akiwa katika picha na Wazee wanaolelewa katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza cha Tushikamane Pamoja Foundation yaliyopo Kata ya Kwembe, Manispaa ya Ubungo mkoani Dar Es Salaam tarehe 15 Oktoba, 2025 wakati wa ziara yake katika Makazi hayo .
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt John Jingu akipokea tuzo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mchango wake katika uboreshaji huduma za ustawi wa Jamii wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Ustawi wa Jamii katika Viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama Dar Es Salaam Agosti 30, 2025.