Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

Usajili wa Makao ya Watoto

VIAMBATISHO VYA USAJILI WA MAKAO

A: MWOMBAJI  BINAFSI

  1. Barua ya maombi ya leseni  kwenda kwa Mkurugenzi wa Halmashauri
  2. Fomu Na. 2 (a) kwa mwombaji binafsi
  3. Fomu Na. 2(c) ya maoni ya Afisa Ustawi wa Jamii
  4. Barua ya Utambulisho wa Makao kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kata
  5. Taarifa ya Uchunguzi  ya Afisa Ustawi wa Jamii
  6. Taarifa ya Ukaguzi  wa Makao ya  Afisa Afya
  7. Nakala ya cheti  cha  taaluma ya Mtaalam wa Ustawi wa Jamii (Degree  of  Social Work/Sociology/psychology/early childhood development/Theology)

Ratio  Afisa 1: Watoto 45

  1.  Nakala ya cheti  cha taaluma ya  Mlezi wa watoto  (certificate of social work/child care / childhood development)

Ratio umri 0-6 Watoto 5: Mlezi 1, Umri 7-14 20:1, Umri 15-17  25:1

  1. Nakala ya cheti  cha taaluma ya Muuguzi (diploma in clinical medicine) iwapo Makao yatalea watoto wenye mahitaji maalum kama vile wenye ulemavu, magonjwa sugu au wanaoishi na VVU
  2. Mikataba ya ajira ya Watumishi wote katika Makao
  3. Fomu ya Serikali ya Uchunguzi wa Afya ya Mpishi/wapishi  wa Makao
  4. Iwapo Makao yana Mtumishi raia wa kigeni iwasilishwe nakala ya hati ya Ukazi na kibali cha kufanya kazi nchini (Residence permit and Work permit)
  5. Uthibitisho wa vyanzo vya mapato vya uendeshaji wa Makao /Barua ya Mfadhili
  6. Nakala ya Hati Miliki ya eneo au Mkataba usiopungua miaka 3 wa kupanga majengo
  7. Nakala za taarifa za kibenki kwa miezi 3 ya karibuni
  8. Nakala za nyaraka zote  ziwe certified

B: MWOMBAJI TAASISI/SHIRIKA

  1. Barua ya maombi ya leseni  kwenda kwa Mkurugenzi wa Halmashauri
  2. Fomu Na. 2(b) kwa mwombaji  Taasisi/Shirika
  3. Fomu Na. 2(c) ya maoni ya Afisa Ustawi wa Jamii
  4. Nakala ya Cheti cha usajili kwa  mwombaji ni Taasisi/Shirika
  5. Nakala ya Katiba ya Taasisi/Shirika
  6. Barua ya Utambulisho wa Makao kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kata
  7. Taarifa ya Uchunguzi  ya Afisa Ustawi wa Jamii
  8. Taarifa ya Ukaguzi  wa Makao ya  Afisa Afya
  9. Nakala ya cheti  cha  taaluma ya Mtaalam wa Ustawi wa Jamii (Degree  of  Social Work/Sociology/psychology/early childhood development/Theology)

Ratio  Afisa 1: Watoto 45

  1.  Nakala ya cheti  cha taaluma ya  Mlezi wa watoto  (certificate of social work/child care / childhood development)

Ratio umri 0-6 Watoto 5: Mlezi 1, Umri 7-14 20:1, Umri 15-17  25:1

  1. Nakala ya cheti  cha taaluma ya Muuguzi (diploma in clinical medicine) iwapo Makao yatalea watoto wenye mahitaji maalum kama vile wenye ulemavu, magonjwa sugu au wanaoishi na VVU
  2. Mikataba ya ajira ya Watumishi wote katika Makao
  3. Fomu ya Serikali ya Uchunguzi wa Afya ya Mpishi/wapishi  wa Makao
  4. Iwapo Makao yana Mtumishi raia wa kigeni iwasilishwe nakala ya hati ya Ukazi na kibali cha kufanya kazi nchini (Residence permit and Work permit)
  5. Uthibitisho wa vyanzo vya mapato vya uendeshaji wa Makao /Barua ya Mfadhili
  6. Nakala ya Hati Miliki ya eneo au Mkataba usiopungua miaka 3 wa kupanga majengo
  7. Nakala za taarifa za kibenki kwa miezi 3 ya karibuni
  8. Nakala za nyaraka zote  ziwe certified.

C: KUHUISHA LESENI

  1. Viambatisho vyote hapo juu  kwa Kundi A/B
  2. Nakala ya leseni

MUHIMU KWA MAOMBI NA WAOMBAJI WOTE

Maombi na nyaraka zote ziwasilishwe Wizarani kwa barua ya Mkurugenzi wa Halmashauri  yalipo Makao kupitia anwani ya;

KATIBU MKUU,

WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM,

S.L.P 573,

DODOMA.