Maendeleo ya Jinsia
Maendeleo ya Jinsia
Lengo
Idara ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake inajukumu la kuratibu masuala ya jinsia na uwezeshaji wa wanawake na wasichana kwa lengo la kuhakikisha haki na usawa wa kijinsia unafikiwa nchini. Utekelezaji wa idara unaongozwa na Sera ya Taifa ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake ya mwaka 2023, Sheria, Miongozo na Mipango ya Kitaifa na Kimataifa inayohusu masuala ya jinsia.
Majukumu ya Idara
- Kuandaa, kupitia, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa Sera, miongozo na mipango ya Jinsia na Wanawake;
- Kuandaa na kutekeleza taratibu za kuingiza masuala ya jinsia katika sera, mipango, mikakati ya Serikali na kufuatilia utekelezaji wake;
- Kuhimiza utekelezaji wa mikataba ya Kikanda na kimataifa kuhusu jinsia na wanawake;
- Kuratibu matukio na maadhimisho ya Siku za Kitaifa na Kimataifa na kufuatilia utekelezaji wa maagizo, maazimio na makubaliano ambayo nchi imeridhia kuhusu jinsia na wanawake;
- Kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuwawezesha wanawake;
- Kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali wa maendeleo, Asasi za Kiraia, Watafiti na Taasisi za kitaaluma; na
- Kutoa masuluhisho ya kiubunifu kwa Sera, Sheria na changamoto za kiutendaji zinazohusiana na ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya wanawake.