Utawala na Rasilimali Watu
Utawala na Rasilimali watu
Lengo
Kutoa huduma za utaalamu na usaidizi kuhusu Rasilimali Watu na masuala ya utawala Kazi
• Kuratibu masuala ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu kimkakati, kama vile kuajiri, maendeleo ya rasilimali watu na mafunzo, kupandisha vyeo, nidhamu, usimamizi wa utendaji kazi, motisha na ustawi.
• Kumshauri Katibu Mkuu kuhusu masuala ya utawala na matumizi ya rasilimali.
• Kuhakikisha usimamizi na matumizi bora, yenye tija na madhubuti ya rasilimali watu.
• Kukusanya, kuchambua, kuhifadhi na kusambaza data na taarifa zinazohusiana na mipango ya maendeleo ya rasilimali watu.
• Kuhakukikisha uhusiano kati ya Wizara na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma katika utekelezaji wa Sheria za Utumishi wa Umma;
• Kuratibu usimamizi wa data na rekodi za kisasa za taarifa mbalimbali za rasilimali watu;
• Kushughulikia mafao ya mwisho na kustaafu kwa watumishi.
- Sehemu ya Utawala
• Kutafsiri na kuhakikisha uzingatiaji wa Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma na sheria nyinginezo za Kazi.
• Kuwezesha mahusiano na ustawi wa wafanyakazi ikijumuisha afya, usalama, michezo na utamaduni.
• Kusimamia rekodi za ofisi;
• Kushughulikia masuala yote ya itifaki.
• Kuwezesha utoaji wa huduma za usalama, usafiri na huduma za jumla.
• Kuwezesha huduma za matengenezo ya vifaa vya ofisi, jengo na viwanja.
• Kuandaa programu za mafunzo ya wafanyakazi kwa mafunzo ya awali kazini, kozi fupi na ndefu.
• Kutayarisha na kupitia makadirio ya mahitaji ya rasilimali watu;
• Kuendeleza muundo wa kazi kwa wafanyakazi.
• Kubuni, kupanga na kutathmini programu za mafunzo.
• Kuratibu utekelezaji wa shughuli za maadili na kukuza thamani ikiwa ni pamoja na kuzuia vitendo vya rushwa.
• Kutekeleza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na jinsia, ulemavu na VVU/UKIMWI n.k na kuwa Kiini cha Jinsia cha Wizara.
• Kuratibu utekelezaji wa ushiriki wa sekta binafsi katika Wizara.
• Kuratibu utekelezaji wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja katika Sekta.
Sehemu ya Usimamizi wa Rasilimali Watu
• (i) Kuratibu Ajira kwa wafanyakazi, uteuzi, upangaji kazi, uthibitisho, upandishaji vyeo na uhamisho.
• (ii) Kufanya mipango kazi ya rasilimali watu ili kubainisha mahitaji ya wataalamu chini ya Wizara.
• (iii)Kusimamia na kushughulikia mishahara.
• (iv) Kuratibu utekelezaji wa Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS), kutathmini matokeo ya tathmini; kuandaa taarifa za utekelezaji; na kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo kwenye fomu binafsi za OPRAS.
• Kuchakata na kuhuisha rekodi za likizo mbalimbali.
• Kusimamia mafao ya wafanyakazi (pensheni, posho n.k) na stahili.
• Kuandaa Makadirio ya Mwaka ya Mapato ya Wafanyakazi;
• Kusimamia huduma zinazohusiana na kujitenga na huduma (kustaafu, kujiuzulu, nk)
• Kuandaa na kuwezesha utekelezaji wa mirathi.
• Kuwezesha programu elekezi/ujuzi kwa wafanyakazi wapya.
• Kufanya tathmini ya mahitaji ya mafunzo na kuandaa programu za mafunzo kwa Wizara.
• Kuwezesha mafunzo ya Rasilimali Watu na kukuza taaluma (maendeleo ya kitaaluma, uboreshaji wa utendaji kazi, kabla ya kustaafu).
• Kufanya tathmini ya manufaa ya programu za mafunzo na kuandaa taarifa.
• Kuanzisha na kuratibu kozi za ndani na mafunzo ya kazi na kutunza kumbukumbu za mafunzo;
• Kutoa taarifa, ufafanuzi na muhtasari kuhusu masuala ya kibinadamu na mafunzo; na
• Kutumikia kama sekretarieti ya msaada kwa Kamati ya UTEUZI, Kamati ya Mafunzo na Maendeleo ya Kitaalamu itakayoundwa katika Wizara.