Makundi Maalum
MAUDHUI KWA AJILI YA KUELIMISHA UMMA KUHUSU KITENGO CHA MAKUNDI MAALUM
UTANGULIZI
Kitengo cha Makundi Maalum Kimepewa dhamana ya kuratibu na kusimamia shughuli za kiuchumi za wafanyabiashara ndogondogo nchini. Wafanyabiashara hao wamegawanyika katika makundi mbalimbali yanayojumuisha wananchi wanaojihusisha na uzalishaji, biashara na utoaji wa huduma. Miongoni mwao ni Waendesha Bodaboda, Waendesha Bajaji, Wasusi, Madereva wa Teksi, Machinga, Mama na Baba lishe, Wauza Matunda na Mbogamboga, Wauza Nafaka, Wauza Samaki wadogo, Wauza Nyama na Kuku sokoni, Wauzaji wadogo wa Mayai kwa kutembeza, Wauza Kahawa na Kashata, Wauza Vinywaji na juisi, Wauza Nguo na Viatu kwa kutembeza, Wauza Mitumba, Wauza Vipodozi rejareja, Wauza Dawa za Asili, Wafanyabiashara wa maduka madogo (vibanda na vioski), Wamiliki wa Saluni ndogo za kike na kiume, Vinyozi, Washonaji na Mafundi Cherehani, Mafundi Seremala, Mafundi Uashi, Mafundi Umeme, Mafundi Bomba, Mafundi Saa, Mafundi wa Vifaa vya Elektroniki (simu, televisheni, redio na kompyuta), Mafundi wa Magari, Waziba Pancha, Mafundi wa Pikipiki, Mafundi wa Baiskeli, Wachomelea Vyuma, Watengenezaji wa Samani, Wafinyanzi wa Vyungu vya Asili, Wafumaji, Watengenezaji wa Sabuni, Watengenezaji wa Batiki, Watengenezaji wa Mikeka, Vikapu na bidhaa nyingine za mikono, watengenezaji wa Mikate, Maandazi na Vitafunwa vingine, Wauza gesi za Kupikia, Wauza Maji, Wakulima Wadogo wanaouza mazao yao, Wafugaji wadogo, Wavuvi wadogo, Wasindikaji wadogo wa mazao ya Kilimo, Mawakala wa huduma za Fedha kwa njia ya Simu, Mawakala wadogo wa Usafirishaji (courier), Makuli, Mawinga pamoja na Makundi mengine mengi ya wananchi wanaojishughulisha na shughuli za uchumi katika sekta isiyo rasmi.
Uratibu na usimamizi wa shughuli za kiuchumi za wafanyabiashara ndogondogo unalenga kufikia uchumi imara, jumuishi na shindani kwa kuzingatia mwelekeo wa DIRA 2050 ambapo maeneo yanayolengwa ni pamoja na:-
- Mfumo wa Utambuzi, Usajili na Utoaji wa Vitambulisho vya Kidijitali vya Wafanyabiashara ndogondogo (WBN-MIS). Mfumo huo umeweka msingi mzuri wa utambuzi na usajili wa wafanyabiashara ndogondogo kupitia uratibu ngazi ya halmashauri;
- Kuwezesha wafanyabiashara ndogondogo kukua kiuchumi kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu kutoka Serikalini kupitia benki iliyokasimiwa jukumu hilo na Serikali; na
- Kuwaunganisha kwa lengo la kuwapatia elimu ya ujasiriamali/biashara pamoja na kutatua changamoto zao.
MAJUKUMU YA KITENGO CHA MAKUNDI MAALUM
Kitengo cha Makundi Maalum kina majukumu yafuatayo:-
- Kuratibu na kusimamia utambuzi wa Makundi Maalum, Mahitaji yao na Changamoto wanazokabiliana nazo ndani ya jamii na kuzitafutia ufumbuzi;
- Kuratibu na kushiriki kwenye uhuishwaji wa Sera ya Maendaeleo ya Jamii ili kujumuisha masuala ya Makundi Maalum nchini;
- Kuratibu utungaji wa Sheria, kuandaa Kanuni, Taratibu na Miongozo ya uendeshaji wa shughuli za Makundi Maalum nchini;
- Kuratibu uandaaji na utunzaji wa kanzi data ya Makundi Maalum nchini;
- Kuratibu ufuatiliaji na tathmini ya programu mbalimbali za kuendeleza Makundi Maalum nchini;
- Kuratibu na kusimamia uhamasishaji na uelimishaji wa Makundi Maalum kuhusu umuhimu wa kuzingatia sera, sheria, taratibu na kanuni za nchi katika uendeshajiwa shughuli zao za kiuchumi;
- Kuratibu na kusimamia uandaaji wa majukwaa ya kuwakutanisha Makundi Maalum na Wadau wa Maendeleo kwa ajili ya kujadili masuala yanayohusu maendeleo yao na ya nchi kwa ujumla;
- Kuratibu mahusiano ya Serikali na wadau mbalimbali wanao hudumia Makundi Maalum nchini; na
- Kuratibu na kusimamia masuala mtambuka yanayohusu Makundi Maalum.
- UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA KITENGO CHA MAKUNDI MAALUM
|
S/N |
HUDUMA |
MAELEZO YA HUDUMA |
VIELELEZO HITAJIKA |
MUDA NA MALIPO YA HUDUMA |
|
1. |
Utambuzi na sajili wa mfanyabiashara ndogondogo |
Huduma ya usajili inatolewa kwa mfanyabiashara ndogondogo kupita mfumo wa wafanyabiashara ndogondogo (WBN-MIS) |
|
|
|
2. |
Uratibu wa Mkopo wa wafanyabiashara ndogondogo |
Uratibu wa utoaji wa mkopo wenye masharti nafuu, kwa mfanyabiashara ndogondogo mwenye kitambulisho cha kidijital cha mfanyabiashara ndogondogo. |
|
|