Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

Makao ya Taifa ya Watoto Kikombo

  1. UTANGULIZI

Wizara ya Afya, kupitia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na Shirika la ABBOTT FUND TANZANIA wametekeleza kwa pamoja shughuli ya ujenzi wa Makao ya Taifa ya Watoto Kikombo mkoani Dodoma. Makao haya yamejengwa katika eneo la Kikombo kwenye kiwanja Na. 366 kitalu DG katika Jiji la Dodoma chenye ukubwa wa mita za mraba 16004. Makao haya yapo katika kijiji cha Kikombo mnadani kata ya Kikombo Wilaya ya Dodoma Katika Jiji la Dodoma. Makao ya Taifa Kikombo yako umbali wa kilometa 26 kutoka jiji la Dodoma, Kilometa 11 kutoka Ihumwa na kilometa 5 kutoka mji mpya wa Serikali Mtumba. Makao yalizinduliwa na Mh: Makamu wa Rais Dkt Philip Isdory Mpango,  mnamo tarehe 16/6/2021 siku ya mtoto wa Afrika, yakiwa na watoto 28.

  1. MALENGO YA MAKAO

Makao haya yameanzishwa kwa lengo mahususi la kuimarisha huduma za malezi na matunzo kwa watoto wenye uhitaji na kuwandaa kwa ajili ya kuwatengamanisha na familia zao. Aidha Makao haya ya Taifa ya mfano ni moja ya kituo cha utekelezaji wa sayansi ya malezi, makuzi na utengamao wa watoto wanaoishi nje ya familia zao, kukuza vipaji na kutoa elimu ya kujitegemea. 

  1. Makao yanaendeshwa kwa Sheria ya Mtoto Sura ya 13 pamoja na Kanuni za Uendeshaji wa Makao ya Watoto za Mwaka 2012. Serikali inawajibika kutoa huduma zote za msingi kwa watoto wanaoishi kwenye Makao ya Taifa ikishirikiana na wadau mbalimbali.
  2. HUDUMA ZINAZOTOLEWA MAKAO YA WATOTO KIKOMBO.

Huduma zote zitolewazo katika Makao ya Watoto Kikombo ni kwa mujibu wa Kanuni za Uendeshaji wa Makao ya Mwaka 2012 kifungu cha 12 hadi 24 huduma hizo ni;- Malazi, mavazi, malezi, matibabu, chakula na lishe, elimu, ulinzi na Usalama, Usimamizi wa marekebisho ya tabia, uchangamshi wa awali wa watoto wadogo kuanzia miaka 2 hadi 5, stadi za maisha, Utengamao, msaada wa kisaikolojia na Kijamii

 

  1. MAKUNDI YA WATOTO WANAOLELEWA KATIKA MAKAO YA TAIFA KIKOMBO

Makao ya Taifa Kikombo yanalea Watoto yatima, Watoto waliofanyiwa ukatili mbalimbali, Watoto wanaopatwa na majanga ikiwemo kupotea, ajali, wanaoishi na kufanya kazi mitaani, Watoto waliotelekezwa na Watoto wanaoishi katika Mazingira hatarishi. Huduma hizi zinatolewa kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto Sura ya 13 na Kanuni za Makao ya Watoto ya Mwaka 2012.

Makao ya Taifa ya Watoto Kikombo yanahudumia Watoto 177 ambapo watoto  ni wa kike 94 na watoto 82 wa kiume wenye umri kati ya miaka 3 hadi 17. Aidha Makao  haya yana Watumishi 25 na wakandarasi 2 wa huduma ya Usafi 17  walinzi wa kampuni 12 na watu wa kujitolea 6

 

  1. UTARATIBU WA WATOTO KUINGIA NA KUTOKA MAKAONI.

Watoto hupokelewa makaoni kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto sura ya 13 pamoja na kanuni zake za mwaka 2012. Kituo kinapokea Watoto wenye umri wa miaka 2 hadi 17 kutoka katika Halmashauri zote nchini kupitia Ofisi za Ustawi wa Jamii ambapo Watoto hupokelewa kwa hifadhi ya muda. Aidha, Watoto wanaondolewa Makao ni kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 na kanuni zake za mwaka 2012 kwa njia zifuatazo;-

  • Kumuunganisha mtoto na familia yake
  • Kumuunganisha mtoto na mlezi wa kuaminika (Fit person)
  • Malezi ya Kambo(Foster care)
  • Kuasili (Adoption)
  • Kuwapatia watoto wanaomaliza vyuo vya ufundi vifaa vya kuanzia kazi kulingana na fani aliyosomea wakati wa kuwatangamanisha. .
  • Kuwaunganisha na ajira ili waweze kuanza maisha ya kujitegemea.
  • Kuwapatia ushauri/maarifa ya kujiajiri wenyewe.

 

  1. SHUGHULI ZA UZALISHAJI MALI NA MAFUNZO

Makao ya Watoto Kikombo yana eneo maalum lenye ukubwa ekari 15, linalotumika kwa shughuli za uzalishaji katika kilimo.  Makao yanatarajia kuwa na miradi ya ufugaji wa kuku, ng’ombe, samaki. Makao pia yana shughuli za kilimo cha zabibu, miti ya matunda, na mbogamboga (vitunguu, mboga za majani,  na nyanya). Tayari eneo la ekari 3 limetumika kwa kilimo cha mbogamboga, hekari moja miche ya matunda mbalimbali na hekari moja imepandwa Zabibu.

Kituo cha kulelea watoto wadogo mchana (Daycare kinaendelea kutoa huduma kwa watoto wa ndani na nje ya Makao. Kwa sasa kina jumla ya watoto 23(Me 13, Ke 10), ambapo watoto wanaolelewa makaoni ni 7 (Me 5, Ke 2), na 16 (Me 8, Ke 8) ni watoto kutoka nje ya Makao (katika Jamii).

Hata hivyo Makao yanaendelea kubuni miradi mbalimbali itakayosaidia kupunguza utegemezi wa Serikali katika shughuli za uendeshaji. Miradi mingine imependekezwa ikiwemo mradi wa Ukumbi na Chakula.

 

  1. MAJENGO NA MGAWANYO WAKE

Eneo la Makao kuna majengo 18 ambayo ni:-

  • Nyumba 10 za watumishi zenye uwezo wa kubeba watumishi 20-25 pamoja na familia zao, ambapo nyumba 3 zina vyumba 2, nyumba 4 zinavyumba 3 vikiwa na sebule jiko na stoo na nyumba 3 zikiwa na vyumba 4.
  • Mabweni manne, mawili ya watoto wakiume na mawili ya watoto wakike pamoja na watoto wadogo ikiwa na nyumba ya makazi ya mlezi wa watoto, mambweni haya yana uwezo wa kuhudumia watoto 250..
  • Bweni la wasichana lenye uwezo wa kubeba watoto wapatao 100 wenye umri kati ya miaka 5-17 watakaokaa kiumri chini ya miaka 5, 5-10, 11-14, 15-17. Mabwenii yote yana sehemu ya kufulia nguo na kupiga pasi.
  • Jengo la zahanati ambalo litakuwa na wahudumu wa afya wanne, dirisha la dawa, maabara, chumba cha daktari, vyumba vitatu vya mapumziko, chumba cha sindano pamoja na chumba cha upasuaji mdogo.
  • Jengo la maktaba lenye chumba cha kompyuta lenye uwezo wa kuingi za kompyuta 25-30, vitabu, meza, tv au projekta
  • Jengo la utawala lina ofisi ya meneja, ukumbi wa mikutano wenye uwezo wa kuchukua watu 25, ofisi 4 za watumishi 12, vyumba 2 maalum vya mahojiano vyenye kuchukua watoto 6 hadi 8. 
  • Jengo la shule la kulea watoto wadogo mchana (daycare centre) lenye vyumba vya kujifunzia vitatu, uwezo wa kuchukua watoto 20 wenye umri kati ya miaka 4 had 6 na watoto 20 wenye umri kati ya miaka 2 hadi 5. Pia chumba cha michezo na uchoraji kina uwezo wa kuchukua watoto 20, chumba cha watumishi 4, vyoo kwa ajili ya watoto na watumishi. Chumba cha mapumziko na sehemu ya nje ya michezo ya watoto (sandbox, michezo ya kuteleza kwenye majani)
  • Jengo la ukumbi wa mikutano lenye uwezo wa kukaa watu 300, ukumbi wa mkutano wenye jukwaa la maonyesho likiwa na meza pamoja na vyoo
  • Jengo la karakana litakuwa ndio stoo kubwa ya kuweka vifaa vya ufundi, lina eneo ya nje kwa ajili ya mafunzo ya ufundi.
  • Bwalo la chakula lenye uwezo wa kuhudumia watoto 250 kwa wakati mmoja, stoo ya vyombo jiko la gesi la ndani pamoja na jiko la nje.
  • Eneo la michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa kikapu na mpira wa pete

Jengo la vyoo vya nje kwa wanawake, wanaume na pia wenye ulemavu