Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

Mahabusu ya Watoto Arusha

1.0 UTANGULIZI

Mahabusu ya watoto arusha ilianzishwa na serikali mwaka 1974 kwa lengo la kuhifadhi watoto waliokinzana na sheria wakati wakisuburi kesi zao ziamuliwe na mahakama.  Wakati wakisubili kesi zao watoto wanapatiwa huduma ya marekebisho ya tabia ambayo ndio msingi mkuu wa uanzishwaji wa kituo.

Mahabusu ya watoto arusha inauwezo wakuhifadhi watoto hamsini kwa mara moja yani wa kiume arobaini (40) na wa kike kumi (10).

Mahabusu ya watoto arusha ipo mtaa wa bondeni,kata ya kati, tarafa ya themi,katika jiji la arusha na mkoa wa arusha. Mahabusu hii inahudumia wilaya zote za mkoa wa arusha yaani longido, meru, arusha dc, ngorongoro, monduli, karatu na arusha jiji.

2.0 TARATIBU ZA KUPOKEA WATOTO

Watoto wote wanapokelewa kutoka mahakamani wakiwa na hati ya mashtaka baada ya kufunguliwa mashtaka. Pindi tu mtoto anapofikishwa katika mahabusu,kulingana na kanuni za mahabusu za watoto ya mwaka2012,  meneja/ afisa ustawi ataweka kumbukumbu sahihi za mtoto kwenye rejesta mbalimbali. Pia mtoto ataelezwa kanuni na taratibu za mahabusu ili aweze kuzifuata.

3.0 HUDUMA ZILIZOTOLEWA KWA WATOTO

  1. Chakula, malazi, mavazi, matibabu.
  2. Ushauri nasihi (msaada wa kisaikolojia)
  3. Elimu ya mabadiliko ya tabia kupitia stadi za maisha.
  4. Huduma za kiroho
  5. Msaada wa kisheria
  6. Kuwezeshwa kuhudhuria mahakamani
  7. Elimu ya stadi za maisha

4.0 MIRADI

Kwa sasa mahabusu ya Arusha haina mradi wowote unaotekelezwa