Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
UTANGULIZI
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kina lengo la kutoa utaalamu na huduma kuhusu matumizi ya TEHAMA katika Wizara. Kitengo kinatekeleza majukumu yafuatayo:-
Majukumu ya Kitengo
- Kutekeleza sera ya ICT na e-Government;
- Kutengeneza na kuratibu mifumo Jumuishi ya ICT kwa ajili ya matumizi ya Wizara.
- Kuhakikisha kwamba maunzi (hardware) na programu za kompyuta vinatunzwa na kuendelezwa vyema.
- Kuratibu na kutoa msaada katika ununuzi wa programu na maunzi (hardware) katika Wizara;
- Kuanzisha na kuratibu matumizi ya mawasiliano ya barua pepe kwenye LAN na WAN.
- Kufanya tafiti na kupendekeza maeneo ya kutumia TEHAMA kama chombo cha kuboresha utoaji wa huduma katika Wizara.
Muundo wa Kitengo
Kitengo cha TEHAMA ni kitengo kinachojitegemea. Kitengo kina jumla ya watumishi sita kikiongozwa na Mkuu wa Kitengo. Kitengo hiki kinawajibika kwa katibu Mkuu wa Wizara