Makao ya Watoto Kurasini
1.0 Utangulizi
Makao ya Watoto kurasini yanaendeshwa kwa Mujibu wa Sheria ya Mtoto
Sura ya 13 Marejeo ya mwaka 2019 na kanuni zake ikiwemo Kanuni ya
Makao ya Watoto za Mwaka 2012 na Kanini ya Ulinzi na Usalama ya
Mtoto.
Makao haya yalianzishwa mwaka 1966 na wamissionari wa Kijerumani
kwa lengo la kulea watoto yatima waliokosa matunzo katika familia. Aidha,
ilipofika mwaka 1968 kituo kilikabidhiwa rasmi kwa Serikali na kusimamiwa
na Idara ya Utawi wa Jamii iliyopo Chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
1.1 Ukubwawa eneo
Makao ya Kurasini yana ukubwa wa hekari tatu na nusu(3.5) ambayo
hutumika kwa shughuli mbalimbali za kuhudumia watoto ikiwemo malazi,
shule ya wali, bwalo la chakula, jiko, ofisi na viwanja vya michezo kwa
kutaja kwa uchache.
1.2 Majengo ya kituo
Makao ya watoto Kurasini yana jumla ya majengo kumi na sita(16)
yanayowezesha utoaji huduma kwa watoto. Ifuatayo ni orodha ya majengo
ya kituo:
i. Jengo la Utawala
ii. Jengo la watoto wadogo na Afisa Mfawidhi(Block)
iii. Jiko
iv. Bwalo la chakula
v. Bweni la watoto wa kike
vi. Bweni la watoto wa kiume
vii. Ukumbi wa shughuli za kijamii
viii. Jengo la kufulia nguo ( Launndry)
ix. Jengo la Walinzi
x. Karakana
xi. Zizi la ng’ombe
xii. Zizi la kuku
xiii. Jengo stationary
Xiv. Jengo la Ktuo cha kulelea watoto wadogo mchana
xv. Vyoo vya nje
Xvi. Mnara wa matank ya maji
2.0 Makundi ya watoto wanaolelewa katika makao ya kurasini
Makao ya Watoto Kurasini yanapokea na kutoa huduma ya malezi kwa
makundi mbalimbali ya watoto walio katikamazingira hatarishi ikiwemo:
i. Watoto yatima waliokosa walezi katika familia
ii. Watoto waathiriwa wa vitendo vya ukatili
iii. Watoto wenye ulemavu na magonjwa ya kusendeka
iv. Watoto waliotelekezwa
v. Manusura wa usafirishaji haramu wa binadamu
vi. Manusura wa vitendo vya utumikishwaji
vii. Watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani
2.1 Huduma zinazotolewa katika Makao
Kituo kinatoa huduma mbalimbali ili kuwawezesha watoto kukua katika
Nyanja zote kimwili, kiakili, kijamii na kiimani. Huduma zinazotolewa ni
pamoja
i. Chakula,
ii. Malazi,
iii. Mavazi,
iv. Afya/matibabu
v. Elimu na mafunzo ya stadi
vi. Uchangamshi wa awali kwa watoto wadogo
vii. Michezo,
viii. Msaada wa Kisaikolojia na
ix. Huduma ya utangamano na kuwaunganisha watoto na familia zao
2.2 Uwezo wa Kituo kupokea watoto
Makao haya yanaweza kupokea jumla ya watoto 85 (Me 42 na Ke 43) idadi
hii imekuja kutokana na nafasi ya vyumba vinavyo patikana katika kituo.
2.3 Idadi ya watoto
Makao haya kwa sasa yana jumla watoto 74 (ME 59, KE 15) na miongoni
mwao watoto 18 (ME 13, KE 7) ni watoto wenye mahitaji maalum
(walemavu).
4.0 Fursa zilizopo
Kituo kina fursa mbalimbali za kuwezesha kuboresha hali ya utoaji wa
huduma:
(i)Uwepo wa ardhi ( ekari 3.5) ambayo inatosheleza ujenzi wa nyumba za
watumishi , zahanati ya kituo na kichoma taka.
(ii)Wadau wa maendeleo ikiwemo wafanya biashara, taasisi za dini na
mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi ambao wanaweza
kushirikisha katika kuchangia juhudi za serikali katika kuboresha
miundombinu na huduma kwa watoto
(iii)Uwepo wa banda la kufugia kuku linaloweza kutumika kuanzisha mradi
mkubwa wa ufugaji wa kuku. ( Andiko la mradi limeandikwa la ufugaji wa
kuku lenye thamani ya TZS. 8, 167,000/=).
(iv)Vijana manusura wa maisha ya mitaani ni rasilimali muhimu katika
kuendelesha miradi ya kituo sambamba na kujifunza stadi za maisha
ikiwemo ufugaji na kilimo cha bustani.
(V) Kituo kimetenga eneo dogo la shamba darasa ambapo watoto
wanajifunzia kulima mboga na matunda kwaajili ya watoto wenyewe.
5.0 Hitimisho
Makao ya Watoto Kurasini ni kituo muhimu katika utoaji wa huduma kwa
makundi mbalimbali ya watoto walio katika mazingira Hatarishi. Aidha, kutokana
na kukua kwa mkoa wa Dar Es Salaam na Halmashauri zake kunasababisha
changamoto nyingi za kijamii hasa watoto wanaoishi katika mazingira Hatarishi;
ambapo baadhi yao wanahitaji kupata hifadhi katika makao haya.