Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

Mahabusu ya Watoto Moshi

Mahabusu ya Watoto Moshi

S.L.P 597 MOSHI

Halmashauri-Moshi Manispaa, Kata-Kiusa, Mtaa-Kiusa Line.

1.0 HISTORIA

Mahabusu ya Watoto Moshi ni Taasisi/kituo cha Serikali ambacho kiko chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu ikisimamiwa na Idara ya Ustawi wa Jamii.  Kituo kilijengwa mwaka 1968 na kilianza kutumika/kufanya kazi mwaka 1970. Kituo hiki cha Mahabusu ya Watoto kinapatikana katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Kata ya Kiusa, Mtaa wa Kiusa Line.

Lengo la kuanzisha kwa mahabusu hii ya watoto ni kuwapatia watoto waliokinzana na sheria ulinzi, malezi na hifadhi salama wakati mashauri yao yakiendelea mahakamani.  Mahabusu hii inaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto Na 21 ya Mwaka 2009 iliyofanyiwa mapitio Mwaka 2019 Kifungu cha 132(8). Na kanuni zake, pamoja na sheria na kanuni pia kuna miongozo mbali mbali ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kueleleza na kusaidia utekelezaji wa sheria na kanuni zake kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa watoto waliokinzana na sheria. Mahabusu ya Watoto Moshi ina uwezo wa kuhudumia Watoto hamsini kwa wakati mmoja (ME 40 KE 10).

2.0 TARATIBU ZA KUPOKEA WATOTO

Watoto wanaopokelewa Mahabusu ni wale ambao wanakua na kesi/mashauri Mahakamani na wamekosa dhamana au wale ambao makosa yao hayana dhamana kama vile mauaji na unyang`anyi wa kutumia silaha.  Kipindi watoto wakiwa Mahabusu wanaendelea na mashauri yao Mahakamani. Tunapokea Watoto kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Kilimanjaro.

  1. HUDUMA ZINAZOTOLEWA KWENYE MAHABUSU YA WATOTO MOSHI
  1. Huduma za unasihi,
  2. Huduma ya msaada wa kisaikolojia na afya ya akili
  3. Watoto wanashiriki kwenye kazi za utunzaji wa shamba la mahindi, miti ya Matunda, migomba na bustani za mboga mboga.
  4. Huduma ya marekedisho ya tabia
  5. Huduma ya elimu, stadi za maisha na ufundi
  6. Michezo mbalimbali
  7. Kuwatangamanisha watoto na familia zao pale mashauri yanapomalizika
  8. Huduma za kiroho
  9. Huduma ya mahitaji ya msingii ambayo ni chakula, matibabu, malazi na mavazi

 

Kwa sasa kazi mradi unaofanyika ni kilimo cha mahindi kwenye eneo lenye ukubwa wa ekari moja na nusu.