Ustawi wa Jamii
IDARA YA USTAWI WA JAMII
Lengo kuu
Kutoa huduma za ustawi wa jamii zenye viwango vya usawa, haki, ubora na endelevu kwa wananchi hususan makundi maalum.
Malengo mahususi
Katika kukuza ustawi wa watu walio katika mazingira hatarishi, familia, vikundi na jamii, pamoja na kuongeza ushiriki wao kupitia sera, mipango na huduma zinazozingatia maslahi ya wateja.
Yafuatayo ni malengo mahususi ya Idara ya Ustawi wa Jamii:
i.Kuandaa, kusimamia na kupitia sheria, kanuni, miongozo kuhusu haki na ustawi wa watu walio katika mazingira hatarishi nchini.
ii. Kumarisha malezi, matunzo na ulinzi wa Watoto walio katika mazingira hatarishi ikiwa ni pamoja na huduma za malezi ya kambo, uasili na usuluhishi wa ndoa zenye migogoro.
iii.Kuimarisha mifumo na utoaji wa huduma kwa watoto walio katika mkinzano na sheria na wale walio katika hatari ya kukinzana na sheria.
iv.Kuimarisha huduma bora katika Vituo vya kulelea watoto mchana, Vituo vya watoto wachanga ikijumuisha vituo vinavyomilikiwa na jamii.
v.Kuratibu, kuongoza, kusimamia na kufuatilia Programu za kijamii za marekebisho ya tabia kwa watoto walio katika mkinzano na sheria ikijumuisha watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.
vi.Kuimarisha malezi, matunzo na ulinzi kwa wazee katika familia, jamii; na katika makazi ya wazee wasiojiweza kama hatua ya mwisho baada ya njia nyingine kushindikana.