Shule ya Maadilisho Irambo
SHULE YA MAADILISHO
Shule ya Maadilisho ni Kituo kilicho chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kinachohudumia watoto ambao wamekinzana na sheria kwa lengo la kumsaidia mtoto aweze kubadilika kitabia akiwa chini ya uangalizi wa Afisa Ustawi wa Jamii na kujifunza stadi za kazi. Ilianzishwa mwaka 1937 kwa Sheria ya watoto na watu wa umri mdogo na baadae kusimamiwa na kuendeshwa kwa mujibu wa sheria ya mtoto sura ya 13. Kwa sasa kuna shule ya maadilisho 1 nchini. Kituo hii kinapokea Watoto ambao Mahakama imetoa amri wapelekwe katika shule ya Maadilisho. Aidha Shule ya maadilisho inapokea watoto walio katika ngazi ya elimu ya Msingi na Sekondari.
MAKOSA YANAYOPELEKEA WATOTO KUKINZANA NA SHERIA
- Wizi
- Unyang’anyi kwa kutumia silaha
- Ubakaji na Ulawiti
- Uzururaji
- Mauaji
- Kuhusishwa na nyara za Serikali
- Makosa mengine ya jinai.
HUDUMA ZINAZOTOLEWA KATIKA SHULE YA MAADILISHO
- Kupokea na Kuhifadhi Watoto waliokinzana na sheria ambao Mahakama imetoa Amri ya kwenda shule ya Maadilisho.
- Kutoa huduma za msingi kwa watoto ikiwemo chakula, malazi, mavuzi pamoja na elimu.
- Huduma ya unasihi.
- Kutoa huduma za malezi, makuzi na maendeleo katika kipindi chote wanapokuwa katika mahabusu.
- Kurekebisha tabia na kuhakikisha wanaunganishwa na familia zao pale mashauri yanapomalizika.
- Huduma ya Afya ya Akili na Msaada wa kisaikolojia Kijamii.
- Stadi za kazi na stadi za maisha.
- Huduma za kiroho.