Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

Ukaguzi wa Ndani

Madhumuni ya Ukaguzi wa Ndani

Lengo kuu la ukaguzi wa ndani ni kutoa huduma za uhakiki huru na za kitaalamu zinazolenga kuongeza thamani na kuboresha utendaji wa shughuli za Wizara. Hii inahusisha kutathmini kiwango cha kutosha na ufanisi wa mifumo ya udhibiti wa usimamizi katika shughuli za kifedha na kiutendaji za Wizara. Huduma hizi za uhakiki husaidia Wizara kufikia malengo yake kwa kutumia mbinu za kimfumo na za kitaalamu katika kutathmini na kuboresha ufanisi wa usimamizi wa vihatarishi, udhibiti wa ndani na mifumo ya utawala bora.

Majukumu ya Huduma ya Ukaguzi wa Ndani

Huduma ya ukaguzi wa ndani itakuwa na majukumu yafuatayo:

a) Kukagua na kutoa taarifa kuhusu uwepo wa udhibiti sahihi wa upokeaji, utunzaji na matumizi ya rasilimali zote za taasisi ya sekta ya umma;

b) Kukagua na kutoa taarifa kuhusu ufuataji wa taratibu za kifedha na kiutendaji zilizowekwa na sheria, kanuni au maelekezo yanayosimamia mapato na matumizi ya taasisi ya sekta ya umma;

c) Kukagua na kutoa taarifa kuhusu uainishaji sahihi, ugawaji na matumizi ya hesabu za mapato na matumizi;

d) Kukagua na kutoa taarifa kuhusu uaminifu na usahihi wa taarifa za kifedha na kiutendaji zinazotumika katika kuandaa taarifa za fedha;

e) Kukagua na kutoa taarifa kuhusu mifumo iliyowekwa kwa ajili ya kulinda mali za taasisi, na inapohitajika kuthibitisha uwepo wa mali hizo;

f) Kukagua na kutoa taarifa kuhusu ukaguzi maalum unaohusu thamani ya fedha (Value for Money), utendaji kazi, usalama wa taarifa, ulinzi wa data, usalama wa mtandao na uchunguzi wa kitaalamu wa udanganyifu (forensic audit);

g) Kukagua na kutoa taarifa kuhusu shughuli au programu mbalimbali ili kubaini kama matokeo yake yanaendana na malengo yaliyowekwa;

h) Kukagua na kutoa taarifa kuhusu utoshelevu wa hatua zinazochukuliwa na menejimenti kufuatia taarifa za ukaguzi wa ndani na nje, pamoja na kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya ukaguzi;

i) Kukagua na kutoa taarifa kuhusu utoshelevu na ufanisi wa mifumo ya udhibiti ndani ya mifumo ya kompyuta ya taasisi ya sekta ya umma;

j) Kukagua na kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa mifumo ya usimamizi wa vihatarishi kila robo mwaka na kila mwaka;

k) Kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa ndani za kila robo mwaka kwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali ndani ya siku thelathini baada ya kumalizika kwa robo husika, baada ya kupitia Kamati ya Ukaguzi na kuidhinishwa na Afisa Masuuli;

l) Kuwasilisha taarifa za mwaka za ukaguzi wa ndani kwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali ndani ya siku thelathini baada ya kumalizika kwa mwaka wa fedha, baada ya kupitia Kamati ya Ukaguzi na kuidhinishwa na Afisa Masuuli; na

m) Kuwasilisha mipango ya ukaguzi inayozingatia vihatarishi kwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali ndani ya siku thelathini kabla ya kuanza kwa mwaka wa fedha, baada ya kupitia Kamati ya Ukaguzi na kuidhinishwa na Afisa Masuuli.

Aidha

Huduma ya ukaguzi wa ndani itafanya yafuatayo:

a) Kukagua utekelezaji wa mifumo ya usimamizi wa vihatarishi kwa msingi endelevu na wa vipindi maalum kama ilivyoainishwa katika mfumo wa usimamizi wa vihatarishi wa taasisi ya sekta ya umma;

b) Kwa lengo la kuboresha usimamizi wa vihatarishi, shughuli za taasisi ya sekta ya umma na kuongeza thamani, kujibu maombi ya msaada au ushauri wa ukaguzi yatakayotolewa na Afisa Masuuli.

Vilevile

Huduma ya ukaguzi wa ndani itatathmini na kutoa mapendekezo yanayofaa kwa ajili ya kuboresha mifumo ya utawala bora katika taasisi ya sekta ya umma kuhusu:

a) Kufanya maamuzi ya kimkakati na kiutendaji;

b) Kukuza maadili na misingi bora ya uadilifu ndani ya taasisi ya sekta ya umma;

c) Kuhakikisha uwepo wa usimamizi madhubuti wa utendaji kazi na uwajibikaji;

d) Kuratibu shughuli na mawasiliano ya taarifa kati ya ngazi za juu za utawala, wakaguzi wa ndani na nje, watoa huduma nyingine za uhakiki pamoja na menejimenti.

 

 

slot gacor