Huduma za Sheria
Kutoa ushauri wa kisheria kwa Wizara, Idara, Vitengo na Taasisi zilizochini ya Wizara juu ya tafsiri ya sheria, mikataba, dhamana, barua ya ahadi na nyaraka zingine za kisheria.
Kutoa ushauri wa kiutaalam katika maandalizi ya muswada wa marekebisho ya Sheria katika Sekta zinazosimamiwa na Wizara na kuyawasilishwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kushiriki katika mazungumzo mbalimbali na mikutano inayohusu utaalam wa kisheria
Kutafsiri Sheria zinazohusu sekta ya Maendeleo na ustawi wa Jamii.
Kuwasiliana na kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Kuendesha mashauri mbalimbali ya madai, usuluhishi au jinai mahakamani yanayohusu Wizara.
Kuwasiliana na kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika masuala yanayohusu maandalizi ya miswada na marekebisho ya sheria, kanuni na sheria ndogo zinazosimamia/zinazogusa Wizara na taasisi zilizo chini ya Wizara