Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

Msaada wa kisaikologia na Jamii

AFYA YA AKILI NA MSAADA WA KISAIKOLOJIA

Afya ya Akili, Msaada wa Kisaikolojia na Kijamii, ni huduma endelevu inayolenga kukidhi mahitaji ya mtu kimwili, kihisia, kijamii, kiroho na kiakili.

Kwanini huduma ya Afya ya Akili, Msaada wa Kisailojia na Kijamii: changamoto za maisha kama vile, Majanga, Ukatili, Migogoro ya ndoa na familia inayosababisha watu kuwa na uwoga, hofu, wasiwasi, msongo wa mawazo, sonona, kupoteza matumaini, kukosa usingizi, kuhisi huna thamani,kujitenga, kuwa na mawazo ya kujiua n.k.

Huduma hii hutolewa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na wizara za kisekta (Wizara ya Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu na OR - TAMISEMI) na Wadau wa Maendeleo kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo.

Watoa huduma ya Afya ya Akili, Msaada wa Kisailojia na Kijamii:

  • Maafisa Ustawi wa Jamii
  • wanasaikolojia
  • Wahudumu wa Afya
  • Maafisa ustawi wa jamii
  • Afisa Uangalizi
  • Viongozi wa Dini
  • Vingozi wa Jadi
  • Walimu
  • Polisi Dawati
  • Watoa huduma ngazi ya jamii
  • Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa Mwanamke na Mtoto
  • Mashirika yanayotoa huduma ya Afya ya Akili, Msaada wa Kisailojia na Kijamii

 

Wanufaika wa huduma ya Afya ya Akili, Msaada wa Kisailojia na Kijamii: mtu mmoja mmoja, Familia, na makundi ya wanajamii wakiwemo:

  • Wazee
  • Watu wenye Ulemavu
  • Watoto walio katika mazingira hatarishi
  • Vijana balehe
  • Wanawake
  • Wanaume
  • Watu wanaoishi na magonjwa sugu
  • Wanafunzi/ wanachuo
  • Watoa huduma

 

HUDUMA ZA AFYA AKILI, MSAADA WA KISAIKOLOJIA NA KIJAMII ZINAPATIKA KWA:

  1. Maafisa Ustawi wa Jamii Ngazi ya Halmashauri
  2. Waratibu wa Afya ya Akili Ngazi ya Halmshari
  3. Walimu wa Malezi na Unasihi Mashuleni
  4. Kamati za Ulinzi na Usalama kwa Mwanamke na Mtoto
  5. Viongozi wa Jamii
  6. Wana Saikologia
  7. Wazazi na  walezi
  8. Polisi wa dawati la jinsia
  9. Viongozi wa Dini
  10.  Walimu wa dini na Madrasa
  11. Watoa huduma ngazi ya Jamii (Community Heath care workers)