Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

HUDUMA KWA WAZEE

HUDUMA KWA WAZEE

  1. HUDUMA KWA WAZEE NCHINI

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wanawake na Makundi Maalum kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii inaratibu na kusimamia huduma zifuatazo kwa wazee ikiwa ni pamoja na: -

  1. Huduma za Matunzo kwa Wazee na Wasiojiweza
  2. Huduma msaada wa afya ya akili na msaada wa Kisaikolojia
  3. Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee Oktoba Mosi
  4. Siku ya Kuelimisha na Kupinga Ukatili Dhidi ya Wazee, 15 Julai
  5. Jamii kufanya maandalizi ya maisha ya uzeen.i
  6. Uanzishwaji wa Klabu za michezo katika ngazi mbalimbali.

 

  1. SERA, SHERIA, MIONGOZO NA MIKAKATI INAYOSIMAMIA HUDUMA KWA WAZEE:
  1. Sera ya Taifa ya Wazee ya Mwaka 2003
  2. Sera ya Taifa ya Afya 2007
  3. Mwongozo wa Uanzishwaji na Uendeshaji wa Makazi ya Wazee na Wasiojiweza 2019
  4. Mwongozo wa Uanzishwaji na Uendeshaji wa Mabaraza ya Ushauri ya Wazee 2023
  5. Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee nchini

 

  1. MATUNZO KWA WAZEE NA WASIOJIWEZA

Katika eneo la matunzo ya wazee Idara inasimamia na kutoa huduma ya matunzo kwa wazee waliko katika Makazi ya Serikali 13 nchini. Pia, inafanya usimamizi na ufuatailiaji wa utoaji wa huduma kwa wazee wanaopata matunzo katika Makazi ya Wazee ya Binafsi 15.

Wizara inatoa Usajili kwa Makazi ya Wazee ya Binafsi ambayo yanaweza kumilikiwa na mtu binafsi, asasi zisizo za Serikali, mashirika ya kijamii, mashirika ya dini, mifuko maalum, Serikali kuu, Serikali za mitaa,au umoja wa washirika.

  1. HATUA ZA UANZISHAJI WA MAKAZI
  1. Kuwasasilisha Barua ya maombi katika Ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ambako makazi yanalengwa kuanzishwa akiambatishwa na barua ya utambulisho kutoka Ofisi ya Mtendaji wa Kata, nakala ya Katiba iliyoidhinishwa na aidha Kabidhi Wasihi Mkuu, Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali/ Usajili wa Vyama vya Kiraia, pamoja na nakala ya hati ya usajili.
  2. Afisa Ustawi wa Jamii atafanya usaili wa kijamii kwa mwombaji, uchunguzi wa kijamii utakaojumuisha kutembelea majengo, kukagua mazingira, kuhoji wadhamini na watu wengine muhimu ili kuandaa taarifa ya uchunguzi wa kijamii.
  3. Afisa wa Afya wa Halmashauri atakagua makazi na ataandika taarifa ya ukaguzi wa mazingira na kuiwasilisha kwa Afisa Ustawi wa Jamii
  4.  Afisa Ustawi wa Jamii atawasilisha maombi kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii yaliyoambatishwa na taarifa ya usaili, taarifa ya uchunguzi wa kijamii na taarifa ya ukaguzi wa kiafya na mazingira    
  5. Ofisi ya Kamishna wa Ustawi wa Jamii itachambua maombi na endapo hayatoshelezi masharti yatarudishwa kwa Afisa wa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri kwa ufafanuzi zaidi na marekebisho.
  6. Kamishna atatoa kibali cha kuanzisha na kuendesha makazi ya wazee na wasiojiweza endapo maombi yatatimiza masharti yanayotakiwa,
  7. Muda wa kushughulikia maombi na utoaji wa kibali kwa Halmashauri ni siku kumi na nne (14) na Siku 7 kwa Wizara kutoa kibali.Muda wa Kinabali kibali ni miaka miwili baada ya hapo kitahuishwa.Sifa za mtu anayestahili kupokelewa na kupewa hifadhi katika Makazi .

 

  1. SIFA ZA MATUNZO WAZEE KUPATA MATUNZO
  1.  Awe Mtanzania
  2.  Awe ni mzee asiyejiweza na amekosa matunzo katika familia na jamii
  3.  Awe mtu asiyejiweza
  4.  Awe ameomba yeye mwenyewe au kuombewa kupitia Mamlaka za     Serikali za Mitaa/Kijiji
  5. Awe amefanyiwa uchunguzi wa kina wa Kijamii na Afisa Ustawi wa Jamii wa eneo husika na kuthibitika kuwa ana sifa za kupata hifadhi, matunzo na ulinzi katika makazi ya wazee
  6. Awe amefanyiwa uchunguzi wa kina wa hali ya afya.