Maendeleo ya Mtoto
Maendeleo ya Mtoto
Lengo Kuu
Kuhakikisha utekelezaji wa haki tano za Mtoto kama zilivyoainishwa katika Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya mwaka 2008 ambazo ni haki ya kuishi kwa mtoto bila kukatisha uhai wake, haki ya kuendelezwa kielimu na vipaji vya mtoto, haki ya kulindwa dhidi ya ukatili wa aina yoyote, haki ya kushiriki kwa mtoto katika masuala yanayomuhusu kwa umri wake na haki ya kutobaguliwa kwa mtoto kutokana na hali yake.
Majukumu
- Kuendeleza, kuratibu na kutathmini utekelezaji wa Sera, Sheria; Mikakati, Programu na Miongozo inayohusiana na watoto, malezi na familia Mfano Sheria ya Mtoto. Na.21 (2009)
- Kuratibu maandalizi na kuwasilisha taarifa za Nchi za Utekelezaji wa Mikataba, Itifaki na Maazimio ya Kimataifa na Kikanda kuhusu haki za mtoto kama vile Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto (CRC) na Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto (ACRWC)
- Uratibu wa utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi na Makuzi ya Awali (PJT- MMMAM) ya mtoto wa miaka 0-8 kipindi ambacho ukuaji wa ubongo wa binadamu hufikia asilimia 90 ya ukuaji wake
- Uratibu na usimamizi wa programu za kuelimisha wazazi au walezi na jamii katika kuimarisha wajibu wao katika malezi chanya ya watoto na familia kupitia programu ya “Familia Bora, Taifa Imara”
- Kujengea uwezo maafisa wa serikali kuhusu uanzishaji wa vikundi vya malezi chanya katika ngazi ya jamii ili kuimarisha elimu ya malezi ya watoto kupitia vikundi katika ngazi ya msingi
- Uratibu katika uanzishaji na kuimarisha Mabaraza ya Watoto katika ngazi ya Kijiji/Mtaa hadi Taifa likiwa ni jukwaa la watoto la kuwashirikisha watoto masuala yanayowahusu kwa umri wao
- Uratibu wa uanzishaji wa Madawati ya Ulinzi na Usalama wa Watoto katika shule za msingi na sekondari ikiwa ni fursa ya watoto kujengeana uwezo wa kujilinda na vitendo vya ukatili
- Uratibu wa kampeni za Kitaifa za kutokomeza ukatili dhidi ya watoto ikiwa pamoja na ukeketaji, mimba na ndoa za utotoni, ukatili wa watoto kupitia mitandao na katika tasnia ya sanaa
- Kufuatilia na kufanya tathmini ya Simu ya Msaada ya Bure kwa ajili ya kutolea taarifa ya vitendo vya ukatili (CHL 116) shuleni, nyumbani na katika jamii
- Kuratibu tafiti sambamba na kuweka utaratibu wa kukusanya, kusambaza na kudhibiti matumizi ya taarifa kwa ajili ya maendeleo ya watoto na familia
- Kushirikiana na wadau wa Maendeleo wa ndani na nje ya Nchi katika kutekeleza afua mbalimbali kwa kuzingatia Sera,Sheria,Kanuni,Miongozo na taratibu za Nchi kama Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya 2008 na Sheria ya Mtoto Na. 21 ya 2009
SERA
- Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya Mwaka 2008
SHERIA
- Sheria ya Mtoto Na 21 ya Mwaka 2009 iliyofanyiwa maboresho mwaka 2019
MIONGOZO
- Mwongozo wa Taifa wa Uundaji na Uendeshaji wa Mabaraza ya Watoto Tanzania
- Mwongozo wa Kitaifa Dawati la Ulinzi na Usalama Mtoto Ndani na Nje ya Shule
- Mwongozo wa Taifa wa Wajibu wa Wazazi/Walezi katika Malezi na Matunzo ya Familia nchini Tanzania
- Mwongozo wa Uratibu wa Programu Jumuishi ya Taifa Ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto
- Mwongozo wa Wawezeshaji wa Programu ya Mahusiano ya Wazazi/Walezi na Vijana Balehe wa Miaka 10-17
PROGRAMU & AJENDA
- Programu Jumusihi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) 2021/22-2025/26
- Ajenda ya Kitaifa ya Kuwekeza katika Afya na Maendeleo ya Vijana Balehe (2021/22-2024/25)
MIPANGO NA MIKAKATI
- Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukeketaji na Mpango wa Utekelezaji wa mwaka 2020/21-2024/25
- Mpango wa Utekelezaji wa Ajenda ya Kitaifa Kuwekeza katika Afya na Maendeleo ya Vijana Balehe ( 2023/24-2024/25)
- Mkakati wa Kitaifa wa Uchechemuzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto
VIJARIDA
- Kijarida cha kuelimisha Wazazi, Walezi na Walimu kuhusu Usalama wa Mtoto Mtandaoni
- Kijarida cha kuelimisha Watoto kuhusu Usalama wa Mtoto Mtandaoni