Usajili na Uratibu wa NGOs
Usajili na Uratibu wa NGOs
SEHEMU YA URATIBU NA UFUATILIAJI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI
Majukumu ya Sehemu ya Uratibu na Ufuatiliaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni pamoja na:
- Kuratibu shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuanzia katika ngazi ya Wilaya, Mkoa hadi Taifa;
- Kufanya ufuatiliaji wa shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kubaini uzingatiaji wa sheria kanuni na miongozo;
- Kufanya tathmini ya utendaji kazi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali;
- Kufanya uchambuzi wa taarifa za utekelezaji na taarifa za fedha za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali;
- Kuweka mazingira wezeshi ya utendaji kazi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali;
- Kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali, Washirika wa Maendeleo, Sekta Binafsi, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Jamii kwa ujumla; na
- Kuhamasisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutekeleza shughuli zao kwa kuzingatia vipaumbele vya Taifa.
SEHEMU YA USAJILI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI
Majukumu ya Sehemu ya Usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni pamoja na:
- Kuandaa na kufanya mapitio ya sera, sheria, kanuni na miongozo inayosimamia shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali;
- Kufanya uchambuzi wa maombi ya usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na kushauri hatua stahiki;
- Kufanya uchambuzi mikataba ya ufadhili yenye kiasi kuanzia shilingi 20 milioni na kuendelea na kushauri hatua stahiki;
- Kutoa mafunzo ya kuyajengea uwezo Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuhusu sera, sheria, kanuni na miongozo inayosimamia shughuli za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali;
- Kufanya tathmini na kushauri kusimamishwa au kufutiwa usajili wa kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali; na
- Kutunza kanzidata ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yaliyosajiliwa na kutekeleza shughuli zake kwa upande wa Tanzania Bara.