Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

Historia

HISTORIA YA WIZARA

 

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ilianzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan mnano tarehe 10 Januari, 2022 baada ya kuitenganisha kutoka iliyokuwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

1.1 Majukumu

Kwa mujibu wa Tangazo la Serikali na 57A na 57B la tarehe 24 Januari 2022, Majukumu ya Wizara yanajumuisha: Maendeleo na utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wanawake, Wazee, Watoto na Makundi Maalum. Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Ukuzaji wa usawa wa Kijinsia, Kutokomeza ukatili wa Kijinsia, Uratibu wa Mashirika ya Kimataifa chini ya sekta hii Uboreshaji wa Utendaji na Maendeleo ya Rasilimali Watu; na Kufanya kazi kwa kushirikiana na Idara nyingine za Wizara, Mashirika ya Umma, Wakala, Programu na Miradi chini ya Wizara hii.