Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko akimkabidhi tuzo Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima kutoka Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) kwa kutambua mchango wake katika Kada hiyo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wataalam hao uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Mei 7, 2025 jijini Dodoma.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, akizindua rasmi huduma za Mahabusu ya Watoto mkoani Mtwara tarehe 12 Aprili 2025. Uzinduzi huu ni hatua muhimu katika kulinda haki za watoto, kuwapatia elimu, na kuimarisha mifumo ya ulinzi na ustawi wao.
Waziri wa Maendeleo ya Jamiii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima katika Hafla ya kupokea nakala ya Vitabu vya Mwongozo wa uundaji na uratibu wa Jukwa la uwezeshaji wanawake kiuchumi,April 08, 2025 - Dar es Salaam, April 08, 2025 - Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwananidi Ali Khamis, akishiriki futari na watoto wanaolelewa katika kituo cha Taifa Kikombo. Futari hiyo imeandaliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Machi 25, 2025 katika makao ya kulea watoto Kikombo.
Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu akishiriki katika Mkutano wa kimataifa unaohusisha wajumbe wa nchi jumuiya za umoja wa kimataifa kwa lengo la kujadili nafasi ya mwanamke katika nchi zao ikiwa ni miaka 30 baada ya maazimio ya Beijing Machi 13, 2025 Jijini New york Marekani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongea na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (Mb) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Sheikh Abeid Amri kwa mkoani Arusha ajili ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Machi 8, 2025
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (Mb), akisalimiana na wananwake wakati wa wa Kongamano laWananwake kanda ya Ziwa lililofanyika Machi 2, 2025, mkoani Geita.
Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Dkt. Stargomena Tax akiwa na viongozi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wanawake na Makundu Maalum, Viongozi wa Mkoa wa Arusha pamoja na wageni Waalikwa kwenye Kongamano la Wananwake kanda ya Kaskazini lilifanyika Machi 6, 2025 Kwenye ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) akihutubia kwenye Kongamano la Wanawake wa nyanda za Juu Kusini lililofanyika March 5, 2025 Mkoani Mbeya.