Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

FURSA ZA MIKOPO WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO

31 Jan, 2026 Pakua

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu
Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Wizara ya Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, inaendelea kutekeleza dhamira
yake ya kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa vitendo.


Kwa muktadha huo, ninapenda kutumia fursa hii kuwaalika na kuwahamasisha
wafanyabiashara ndogondogo wote ku changamkia fursa ya mikopo ya Serikali
yenye masharti nafuu na riba ya asilimia saba (7%) kwa mwaka inayotolewa
kupitia Benki ya NMB ambayo ime ingia makubaliano na Serikali kusimamia mikopo
hiyo.