Uhasibu
Uhasibu
- Lengo
- Kusimamia matumizi sahihi ya fedha na kutunza taarifa za fedha za Wizara
- Majukumu
- Kusimamia matumizi sahihi ya fedha za Serikali;
- Kushauri Menejimenti kuhusu sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya fedha za Serikali na kusimamia ukusanyaji mapato ya Serikali kwa Fungu 53;
- Kukusanya na kuwasilisha maduhuli ya Serikali kwa niaba ya Mlipaji Mkuu wa Serikali;
- Kusimamia na kuhasibu fedha zote za Wizara zinazotolewa na Serikali na Wadau wa Maendeleo kwa mujibu wa Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge la Tanzania;
- Kuandaa taarifa mbalimbali za Fedha na Kihasibu ikiwa ni pamoja na Hesabu za Wizara (Fungu 53), Taarifa za Robo na Nusu Mwaka, kujibu hoja za ukaguzi, kwa kufuata sheria kanuni na miongozo na kuwasilisha sehemu husika kwa wakati; na
- Kutunza nyaraka za fedha na uhasibu kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Umma, Sura 348