Mawasiliano Serikalini
Mawasiliano Serikalini
KAZI ZA KITENGO
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kina jukumu la kutoa ushauri wa kitaalamu na huduma katika masuala ya Habari na Mawasiliano kwa Wizara.
Lengo ni kuhakikisha utekelezaji wa malengo ya Wizara unajulikana kwa Umma, kupitia Habari, Elimu na Mawasiliano kwa njia ya usambazaji wa habari za wizara kwa wakati, kupokea mrejesho na maoni kutoka kwa wadau
MAJUKUMU YA KITENGO
- Kuandaa na kutekeleza Mkakati wa Mawasiliano.
- Kuzalisha na kusambaza machapisho, nyaraka, makala, vibango ili kuufahamisha umma juu ya sera, mipango, mikakati, utekelezaji na mafanikio ya Wizara,
- Kuratibu mikutano na taarifa kwa Vyombo vya Habari kuhusu Wizara na Taasisi zake.
- Kusimamia shughuli za Mahusiano ya Umma na Huduma kwa Wateja.
- Kushiriki katika mazungumzo, mijadala ya umma na vyombo vya habari juu ya masuala yanayohusu Wizara.
- Kuratibu na kufanya maandalizi ya warsha, mikutano na makongamano ya Wizara;
- Kusimamia na kuhuisha maudhui ya tovuti ya Wizara pamoja na mitandao mingine ya kijamii ya Wizara;
- Kushirikiana mara kwa mara na Maafisa Habari katika taasisi zilizo chini ya wizara kwa ajili ya kupata nyaraka na taarifa mbalimbali kwa lengo la kutoa taarifa kwa ajili ya umma.