Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA UENDESHAJI YA TAASISI YA MAENDELEO YA JAMII TENGERU

29 Jun, 2026 Pakua

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (Mb), anautangazia umma kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 19(1) cha Amri ya Uanzishwaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru ya mwaka 2013, amemteua Dkt. John Elton Lusingu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uendeshaji ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kwa awamu ya pili.


Uteuzi wa Dkt. Lusingu umeanza rasmi tarehe 22 Mei, 2026.

slot gacor