Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

WAZIRI DKT. GWAJIMA AZINDUA CHUO CHA UFUNDI STADI KWA WASICHANA SIMANJIRO, AWATAKA WAZAZI KUTOWANYIMA WASICHANA FURSA YA ELIMU

Imewekwa: 23 Nov, 2026
WAZIRI DKT. GWAJIMA AZINDUA CHUO CHA UFUNDI STADI KWA WASICHANA SIMANJIRO, AWATAKA WAZAZI KUTOWANYIMA WASICHANA FURSA YA ELIMU

Na WMJJWM, MANYARA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, amezindua rasmi Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa Wasichana cha ECLAT kilichopo Emboreet, Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara.  

Dkt. Gwajima akizindua chuo hicho leo Novemba 23, 2026, amewataka wazazi, walezi na viongozi wa mila kuhakikisha watoto wa kike wanapata fursa ya elimu na kuachana na mila zinazowakandamiza. 

Amesema elimu ya ufundi stadi itawawezesha wasichana kupata ujuzi, kujiajiri na kujenga maisha yenye heshima, huku wakichangia maendeleo ya familia na jamii, kwa kutoa mafunzo katika fani za Mapishi na Ushonaji, ambazo zina fursa katika sekta za utalii, huduma na viwanda vidogo. 

Katika hatua nyingine, Dkt. Gwajima amewataka wazazi, walezi na viongozi wa mila kuendelea kudumisha mila njema na kuachana na mila zinazomkandamiza mtoto wa kike, hususan ndoa za utotoni na ukeketaji. 

Naye Mwenyekiti wa ECLAT Development Foundation, Peter Toima Kiroya, ameishukuru Serikali kwa ushirikiano na kuweka mazingira wezeshi kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kushiriki katika shughuli za maendeleo. Aidha, amesema ECLAT itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuendeleza fursa za elimu na mafunzo ya ufundi stadi kwa wasichana, hususani kutoka jamii za wafugaji.

Chuo hicho kimejengwa kati ya mwaka 2024 na 2026 kwa gharama ya shilingi bilioni 1.6 kupitia ushirikiano wa ECLAT Development Foundation na Upendo Association ya nchini Ujerumani, na kimesajiliwa na NACTVET kwa namba REG/NACTVET/1173.

Uzinduzi huo umeambatana na mahafali ya kwanza ya Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa Wasichana cha ECLAT, iliyofanyika katika Kijiji cha Emboreet, Kata ya Emboreet, Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara.

MWISHO

slot gacor