Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

WAZIRI DKT. GWAJIMA AWATAKA WANAWAKE WACHIMBAJI MADINI KUSIMAMIA MALEZI, MAKUZI NA MAADILI MEMA

Imewekwa: 17 Nov, 2026
WAZIRI DKT. GWAJIMA AWATAKA WANAWAKE WACHIMBAJI MADINI KUSIMAMIA MALEZI, MAKUZI NA MAADILI MEMA

Na WMJJWM – Dodoma

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe, Dkt. Dorothy Gwajima amewataka wanawake wachimbaji wa Madini Tanzania (TAWOMA) kusimamia, malezi makuzi na Maadili mema kwa watoto ili kukabiliana na changamoto ya mmomonyoko wa maadili.

Dkt. Gwajima amesema hayo leo 16 Novemba 2026, Jijini Dodoma wakati akifunga mkutano wa mwaka wa Chama chama hicho.

Ameleeza kwamba malezi bora ya watoto ndiyo msingi wa kujenga kizazi cha kesho, hivyo kila mwanamke anatakiwa kuwa mfano wa kuigwa katika usimamizi wa malezi, makuzi na Maadili yenye tija kwa watoto.

‘Naomba muendelee kuhimizana kulea watoto katika misingi ya maadili, juhudi zenu katika kutafuta kipato cha familia kiende sambamba na malezi bora ili, kipato mnachokipata kiwe tija katika familia na jamii kwa ujumla” amesema Dkt. Gwajima

Aidha Mhe, Gwajima ameongeza kwamba Serikali inaendelea kufungua fursa za uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, kuwajengea uwezo wa kusimamia rasilimali, kupata taarifa sahihi, kupata mitaji, kutumia teknolojia, kuendesha biashara na kushiriki katika kufanya maamuzi yanayohusu ili waweze kuwa vinara na wenye mchango katika maendeleo ya Taifa.

‘Nawasihi viongozi wa TAWOMA kuendelea kuimarisha vikundi vya akiba na mikopo, mafunzo ya elimu ya fedha na uwekezaji, afya, usalama migodini na utunzaji wa mazingira. Vilevile, ni muhimu kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi, majukwaa ya maamuzi na michakato ya maendeleo ya Sekta ya Madini” amesema Dkt Gwajima.

Kwa upande wake Mlezi wa Chama hicho Mama Sara Masasi amewataka wanachama hao kuendeleza ushirikiano na taasisi za fedha, serikali na wadau wengine wa maendeleo ili kuhakikisha chama kinakuwa msitari wa mbele na kuhakikisha kila mwanamke anakuwa mnufaika wa fursa mbalimbali za kiuchumi.
MWISHO

slot gacor