Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

SERIKALI NA BENKI YA DUNIA WATATHMINI MRADI WA PAMOJA

Imewekwa: 26 Nov, 2026
SERIKALI NA BENKI YA DUNIA WATATHMINI MRADI WA PAMOJA

SERIKALI NA BENKI YA DUNIA WATATHMINI MRADI WA PAMOJA 


Wataalamu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) na Benki ya Dunia wamekutana  na ili kufanya tathmini ya maendeleo ya Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania (PAMOJA). 

Akizungumza katika tathmini hiyo tarehe 25 Novemba 2026 katika ukumbi wa Mikutano wa St Gasper jijini Dodoma Mratibu wa mradi wa PAMOJA Kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Adventina Kato ameeleza kuwa tathmini hiyo inafanyika kupima utekelezaji wa shughuli za mradi, mafanikio yaliyopatikana na hatua za kuchukua ili kuongeza kasi, ufanisi na ubora wa utekelezaji wa mradi huo.

Ameongeza kuwa utekelezaji wa mradi wa PAMOJA una manufaa kwa jamii kwani umelenga kuwakwamua kiuchumi wanawake hususani wa vijijini pamoja na kupambana na ukatili wa kijinsia na unatekelezwa katika mikoa 10 ya Tanzania bara huku akibainisha baadhi ya shughuli za mradi huo ni utoaji wa mikopo kwa wanawake, ujenzi wa nyumba salama na ujenzi wa vituo vya kulea watoto.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa PAMOJA kutoka TAMISEMI, Linus Kahendaguza ameongeza kuwa TAMISEMI imejipanga kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa ufanisi katika mikoa yenye mradi huo ya Arusha, Mwanza, Kagera, Mara, Singida, Shinyanga, Geita, Rukwa, Tabora na Simiyu.

Naye Mratibu wa Mradi wa PAMOJA kutoka Benki ya Dunia Tanya Delima amesema tathimini hiyo inalenga kuona mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa Mradi huo unaolenga kutokomeza ukatili wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.

slot gacor