Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

WAZIRI DKT. GWAJIMA ASHINDA TUZO YA MALKIA WA NGUVU SEKTA YA UONGOZI BORA

Imewekwa: 15 Nov, 2026
WAZIRI DKT. GWAJIMA ASHINDA TUZO YA MALKIA WA NGUVU SEKTA YA UONGOZI BORA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, ameshinda Tuzo ya Malkia wa Nguvu katika sekta ya Uongozi Bora, iliyotolewa Novemba 14, 2026, kwa kutambua mchango wake katika matumizi ya mitandao ya kijamii kuimarisha mawasiliano na wananchi.
Dkt. Gwajima amejizolea umaarufu mkubwa kupitia matumizi ya majukwaa ya kidijitali kama njia ya mawasiliano ya moja kwa moja na wananchi, akitumia mitandao hiyo kutoa elimu kwa umma, kueleza fursa zinazopatikana kupitia Serikali na kupokea hoja, malalamiko pamoja na changamoto zinazowasilishwa na wananchi.
Ripoti ya Tanzania Civic Space Monitor ya mwaka 2023 ilimtaja Dkt. Gwajima kuwa mfano mashuhuri wa viongozi wanaotumia majukwaa ya kidijitali kupokea malalamiko ya jamii, huku gazeti la The Citizen la Machi 20, 2025, likieleza namna anavyotumia X na Instagram kushirikiana na wananchi.
Mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Dkt. Gwajima ameshukuru kwa heshima hiyo, akieleza kuwa hakutarajia kupata tuzo hiyo kubwa na ya kihistoria. Ameishukuru pia jamii iliyompigia kura na kuahidi kuendelea kutimiza wajibu wake kwa wananchi kwa ari mpya, huku akitoa shukrani kwa @malkiachoicefm @cloudsfmtz @malkiawanguvuaward kwa kuendelea kuiunganisha jamii kupitia Tuzo za Malkia wa Nguvu.
Tuzo hiyo ya Malkia wa Nguvu inatambua mchango wa Dkt. Gwajima katika kuendeleza mawasiliano ya kidijitali na kuimarisha ushiriki wa wananchi katika kuwasilisha hoja na changamoto zao.

slot gacor