Habari

Imewekwa: May, 30 2023

WAZIRI DKT. GWAJIMA AAGANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UNICEF SHALINI BAHUGUNA

News Images

Mei 29, 2023 Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima ameiongoza Menejimenti ya Wizara kumuaga aliyekuwa mwakilishi Mkazi wa shirika la UNICEF nchini Tanzania Shalini Bahuguna katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma.

Waziri Dkt. Gwajima amemshukuru Shalini kwa ushirikiano aliyoipatia Wizara kwa kipindi cha mwaka 2020 mpaka 2023 alichokua akitimiza majukumu yake, hasa kwa kushiriki katika kuhakikisha ustawi na Maendeleo ya watoto Nchini.

Aidha, Waziri Dkt. Gwajima ametumia fursa hiyo kumkabidhi Bi. Shalini zawadi mbalimbali ikiwemo cheti cha kuthamini na kutambua mchango wake.

Kwa upande wake Bi. Shalin licha ya kuishukuru Wizara kwa ushirikiano, ameipongeza kwa utendaji, Ubunifu na uendeshaji wa weledi wa kwenye programu za mbalimbali katika kipindi chote walichokua wakishirikiana kuboresha hali za watoto nchini.

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Wataalam kutoka Shirika la UNICEF Tanzania.