WAZEE WAFURAHIA ZIARA YA KUTEMBELEA MAENEO MBALIMBALI DODOMA
Na WMJJWM- Dodoma
Viongozi na wawakilishi wa Baraza la Ushauri la Wazee Taifa wameeleza kufurahishwa na ujenzi wa miundombinu inayowezesha kutoa huduma mbalimbali jijini Dodoma.
Wazee hao wameeeleza hayo Oktoba 2, 2026 baada ya kufanya ziara ilityoratibiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, kwa lengo la kuwezesha wazee hao kujionea na kujifunza mambo mbalimbali kuhusu miundombinu na vivutio vinavyopatikana jijini Dodoma.
Ziara hiyo ni shemu ya kuadhimisha siku ya Wazee Duniani ambayo hufanyika Oktoba Mosi kila mwaka ambapo kwa mwaka huu kilele chake kitakuwa Novemba 4 mkoani Songwe.
Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Baraza hilo David Sendo amesema Serikali inaendelea kufanya mambo makubwa katika ujenzi wa miundombinu jambo linalorahisiha utoaji wa hduuma bora kwa wananchi.
“Tunampongeza Rais wetu Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika ujenzi wa miundombinu, tumejionea kituo cha treni ya kisasa cha Samia Jijini Dodoma ni kizuri sana na tunafurahishwa na hilo, sisi kama wazee tunatoa wito kwa jamii kuendelea kutunza na kutumia vizuri miundombinu hii kwa maslahi ya Taifa”amesema Mzee Sendo.
Baadhi ya maeneo mengine ambayo wazee hao wamtembela ni Uwanja wa Ndege, Chuo Kikuu cha Dodoma, Mji wa Serikali Mtumba na Hospitali ya Benjamini Mkapa Dodoma