WANAWAKE WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA KUPITIA MAJUKWAA YA UWEZESHAJI KIUCHUMI
Na Saidi Saidi, WMJJWM – Dodoma
Machi 12, 2026
Wanawake wametakiwa kuchangamkia fursa zilizopo katika majukwaa ya uwezeshaji Wanawake kiuchumi Ili kujiongezea kipato kwa Maendeleo yao na kijamii.
Hayo yamesemwa Leo Machi 12,2026, na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamiii Jinsia Wanawake na Makundi Juliana Kibonde, akimwakilisha Mkurugenzi wa Idara hiyo Badru Abdunur, wakati akifungua mafunzo ya uwezeshaji Wanawake kiuchumi kwa Waratubu na Viongozi wa majukwa hayo.
Juliana amewataka waratibu na viongozi wa majukwaa hayo kuhakikisha majukwaa yanatumika ipasavyo kuwaunganisha wanawake na fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo katika sekta tofauti nchini.
Amesema kuwa majukwaa hayo yanaenda sambamba na utekelezaji wa Programu ya Kizazi Chenye Usawa, inayolenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Aidha, amewataka waratibu kuhakikisha majukwaa yanaanzishwa na kuimarishwa katika ngazi zote kuanzia vijiji na mitaa hadi ngazi ya mkoa.
Aidha, amewataka viongozi hao kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa kuhakikisha mikutano ya majukwaa inafanyika mara kwa mara, kutambua fursa zilizopo katika sekta mbalimbali pamoja na kushirikisha wadau wa maendeleo ili kuwasaidia wanawake kukabiliana na changamoto na kuongeza mchango wao katika maendeleo ya familia na taifa.
Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma, Honorata Rwegasila, amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha waratibu na viongozi wa majukwaa kuimarisha utendaji wao katika kusimamia majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi katika ngazi mbalimbali.
Ameongeza kuwa kupitia majukwaa hayo wanawake wanapata fursa ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kuunganishwa na fursa za kiuchumi zitakazosaidia kuboresha maisha yao pamoja na kuchangia maendeleo ya jamii.
Naye Mwenyekiti wa Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Dodoma amewataka wanawake kuendelea kushiriki kikamilifu katika majukwaa hayo ili kujenga umoja na kuimarisha shughuli zao za kiuchum