VITENGO VYA UKAGUZI WA NDANI NA MANUNUZI VYA WIZARA VYAJENGEWA UWEZO KUHUSU MRADI WA PAMOJA
VITENGO VYA UKAGUZI WA NDANI NA MANUNUZI VYA WIZARA VYAJENGEWA UWEZO KUHUSU MRADI WA PAMOJA
Imewekwa: 21 May, 2026
Mratibu wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia na Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia (PAMOJA) kutoka Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Adventina Kato akitoa maelezo kuhusu mradi wa PAMOJA katika kikao kazi cha kuwajengea uwelewa watumishi wa Kitengo vya Ukaguzi wa Ndani na Kitengo cha Ununuzi na Ugavi vya Wizara.
Lengo la kikao kazi hicho ni kuhakikisha watumishi wanauelewa mradi kikamilifu ili waweze kutekeleza majukumu yao kulingana na taratibu za miradi inayopata fedha kutoka Benki ya Dunia.
Kikao kazi hicho cha siku moja kimefanyika leo Mei 20, 2026 katika Ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma