UCHAKATAJI WA TAKA ULIVYOGEUZWA KUWA FURSA YA UWEZESHAJI VIJANA KIUCHUMI.

Na WMJJWM- Dar Es Salaam
Taka za vifungashio vya bidhaa mbalimbali baada ya matumizi ya bidhaa husika, kama vile chupa za Vinywaji, maboksi na mifuko ya simenti zimekuwa fursa ya kiuchumi inayowasaidia vijana wengi Jijini Dar Es Salaam mradi unaotekelezwa na Shirika Lisilo la Kiserikali la Afri Craft.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Kelvin Nicholas amesema hayo Juni 25, 2025, baada ya Timu ya Wataalam wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kutembelea miradi inayotekelezwa na Shirika hilo.
Amesema kupitia mradi wa urejeshaji taka katika bidhaa umesaidia vijana wengi na unasaidia vijana kuinuka kiuchumi, kutunza mazingira, na jamii kwa ujumla kwasababu bidhaa hizo hurudi kwao kwa matumizi mbalimbali.
"Chupa za vinjwaji, maboksi na mifuko ya saruji inayotupwa kwetu ni tursa, vijana hukusamya na kutuletea sisi Kwa ajili ya uchakataji ili kupata bidhaa mpya" amesema Kelvin.
Ameeleza kwamba kwa wiki wa uwezo wa kukusanya tani 12,000 za chupa za Vinywaji zilizotumika ambazo hupelekwa viwandani Kwa ajili ya uzalishaji wa chupa mpya.
Kelvin amesema katika mradi huo wa urejeshaji wa taka umenufaisha vijana wanaofanya kazi mbalimbali, wakiwemo mafundi seremala, wachongaji, na kazi za sanaa.
Jackson Mkuko ni fundi seremala anayefanya kazi katika karakana ya Afri Craft amesema ameendelea kubuni bidhaa mbalimbali zinazotokana na mbao chakavu ambazo zimetupwa.
Baadhi ya bidhaa anazotengeneza ni makontena ya kubebea vinywaji, na kutunzia vitu vya aina tofauti, na urembo wa aina mbalimbali.
Mikakati wa urejeshaji wa taka katika matumizi ya bidhaa ni Mpango endelevu unaosaidia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuendeleza miradi inayogusa jamii na utunzaji wa mazingira.