Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

PIKA ZUNGU: MKUTANO WA WPC NI FURSA KWA TANZANIA.

Imewekwa: 03 Nov, 2026
PIKA ZUNGU: MKUTANO WA WPC NI FURSA KWA TANZANIA.

Na WMJJWM Dar Es Salaam

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) ameeleza kufurahishwa na maandalizi ya Mkutano wa Wabunge Wanawake wa Ukanda wa Maziwa Makuu (WPC), unaofanyika kuanzia tarehe 2 hadi 5 Novemba 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Mhe. Zungu ameeleza hayo tarehe 31 Oktoba 2026 baada ya kutembelea na kufanya ukaguzi wa maandalizi wa eneo la mkutano.

“Tanzania ilikuwa mwenyeji wa Mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Arusha na sasa tunawakaribisha wabunge wanawake katika Ukanda wa Maziwa mlMakuu, hii ni ishara ya kwamba nchi yetu ina amani, utulivu, na uwezo wa kuunganisha watu kwa lengo moja.” amesema Spika Zungu.

Ameongeza kwamba mkutano huu utawezesha wanawake kujadiliana na kushirikina na kutoa sauti kwa maswala ya wanawake, hasa katika maeneo ya kisiasa, elimu, afya, na uwezeshaji wa kiuchumi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo, Mhe. Balozi Thobias Makoba, amesema maandalizi ya mkutano huo yamefikia hatua za mwisho, huku matarajio yakiwa ni kuhakikisha kila mgeni anapokelewa na kuhudumiwa kwa heshima na mkutano unafanyika kwa mafanikio yatakayoliweka Taifa katika kumbukumbu nzuri kwa wageni na waalikwa.

Mkutano huo unatarajiwa kuwakutanisha wawakilishi kutoka nchi 12 za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambapo zaidi ya watu 1,000 wanatarajiwa kushiriki ikiwemo wabunge, wadau wa kisiasa na wataalamu wa uongozi.

slot gacor