Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

NAIBU WAZIRI APONGEZA SHIRIKA LA SOS KWA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI KUMLIMDA MTOTO

Imewekwa: 17 Mar, 2025
NAIBU WAZIRI APONGEZA SHIRIKA LA SOS KWA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI KUMLIMDA MTOTO

Na WMJJWM - Arusha

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwananidi Ali Khamis amelishukuru Shirika la SOS kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuimarisha ulinzi na usalama wa mwanamke na mtoto.

Amesema hayo Machi 15, 2025 akiwa ziarani Wilaya ya Meru, Arusha kwa lengo la kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa programu za malezi mbadala pamoja na programu ya uwezeshaji wa uchumi wa familia na vijana zinazotekelezwa na Shirika la SOS katika Mkoa wa Arusha.

Naibu Wazri Mwanaidi ameomba uongozi wa Shirika hilo kuendelea kushirikiana na Wadau wa Maendeleo kuimarisha jukwaa la wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana pamoja na kamati za MTAKUWWA katika ngazi zote.

"Ninaomba mshirikiane na Uongozi Jukwaa la Wamiliki wa Vituo vya Kulelea Watoto Wadogo Mchana na Kamati ya MTAKUWWA kutatua changamoto zinazowakabili" amesema Naibu Waziri Mwananidi.

Aidha, Naibu Waziri Mwananidi amelipongeza Shirika la SOS kwa kuendelea kushirikiana na Serikali kuimarisha kamati za MTAKUWWA kuanzia ngazi ya Wilaya hadi Vijjijini pamoja na kuwaomba viongozi wa Kamati hizo kutatua changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo kwa kuwapatia mafunzo stahiki ili waweze kutimiza majukumu yao kwa ufanisi mzuri zaidi.