MKURUGENZI CCBRT ATOA USHAURI KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI.

Na WMJJWM- Dar Es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la CCBRT Brenda Msangi ametoa ushauri kwa waendeshaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kuendelea kufanya miradi inayodumu na kugusa jamii.
Brenda amesema hayo Juni 25, 2025 baada ya Timu ya Wataalam wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum kutembelea ofisni kwake Jijini Dar Es Salaam.
Ameyataja mambo muhimu ya kuzingatia kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili yaweze kutekeleza miradi endelevu ni pamoja na kuwa mpango Mikakati wa Mawasiliano kati ya Serikali, jamii na wadau mbalimbali.
"Ni muhimu kuwa na mpango wa namna ya kushirikishana taarifa mbalimbali kutoka kwenye Shirika kwenda kwa Serikali, jamii na wadau, hii inasaidia watu kuelewa huduma zinazopatikana na kutolewa na Shirika husika" anasema Brenda.
Amesema eneo lingine ni ubunifu katika utekelezaji wa miradi pamoja na kupanga namna ya kumaliza mradi unapofikia mwisho na kusisitiza kuwa njia nzuri ya kuachia miradi ni kuhakikisha kuna ushirikiano na Serikali na wadau wengine katika eneo la utekelezaji ili kuikaibidhi miradi hiyo kwao pale ambapo Shirika limefikia mwisho wa utekelezaji wake kwa mujibu wa makubaliano husika.