Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

MASWI ATAKA WATUMISHI KUWAJIBIKA

Imewekwa: 19 May, 2026
MASWI ATAKA WATUMISHI KUWAJIBIKA

Na WMJJWM, Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Eliakim Maswi amewataka watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uwajibikaji ili kuhakikisha huduma bora zinawafikia wananchi na kuleta maendeleo chanya kwa jamii ya Tanzania.

Maswi amezungumza leo Mei 18, 2026 baada ya kupokelewa rasmi na watumishi wa Wizara katika ofisi za Wizara zilizopo Mji wa Serikali Mtumba.

Amebainisha kwamba, ushirikiano, nidhamu na kujituma kwa watumishi ni msingi muhimu wa kufanikisha malengo ya Wizara pamoja na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

“Kila mtumishi anapaswa kutekeleza majukumu yake kwa weledi na uzalendo, huku akihakikisha wananchi wanapata huduma stahiki kwa wakati”

Mapokezi hayo yameongozwa na Waziri Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, akiambatana na Naibu Waziri Marryprisca Mahundi, Naibu Makatibu Wakuu Wakili Amon Mpanju na Felister Mdemu, Wakuu wa Vyuo na Taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na watumishi.

MWISHO

slot gacor