Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

MAENDELEO YA JAMII SPORTS CLUB YANYAKUA MEDALI YA FEDHA SHIMIWI 2026

Imewekwa: 08 Oct, 2026
MAENDELEO YA JAMII SPORTS CLUB YANYAKUA MEDALI YA FEDHA SHIMIWI 2026

Na WMJJWMM - Kilimanjaro 

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi kupitia Klabu yake ya "Maendeleo ya Jamii Sports Club",  imefanikiwa kutwaa Medali ya Fedha katika mashindano ya 40 ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) 2026 yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.

Medali hiyo imepatikana kupitia Mfukuza upepo   Jackline Mbuta aliyeshika nafasi ya pili katika mbio za mita 400 kwa wanawake ambaye ameiletea heshima ya kipekee klabu hiyo.

Hafla ya upokeaji wa Medali hiyo imeshuhudiwa na Mkurugenzi Msaidizi upande wa Utawala kwenye Wizara hiyo,  Apsa Othm ambaye ameshiriki  katika ufungaji na kupokea medali hiyo.

Apsa amewapongeza wanamichezo hao kwa kuiwakilisha vema Wizara kwenye michuano hiyo huku akieleza kuwa Wizara inathamini mchango wao  katika uwanda wa Michezo na inategemea michuano ijayo watafanya vizuri zaidi.

Aidha,  Mwenyekiti wa Klabu hiyo Appolo Daudi ametoa shukurani zake kwa viongozi wa Wizara, kwa kuwawezesha kushiriki mashindano hayo na kuwaunga mkono katika hatua zote huku akieleza kuwa Maendeleo ya Jamii Sports Club ilishiriki katika michezo mbalimbali, ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, bao na karata, huku mpira wa miguu ukifika hatua ya 16 bora, bao wanawake 8 bora na karata 16 bora.

Michezo hiyo imefungwa rasmi Oktoba 7, 2026, huku viongozi wakisisitiza watumishi kuendelea kufanya mazoezi na waajiri kuunga mkono maendeleo ya michezo mahala pa kazi.

MWISHO

slot gacor