DR. JINGU AKUTANA NA UMOJA WA WANAUME TANZANIA

Na WMJJWM- -Dodoma
Ujumbe wa Umoja wa Wanaume Tanzania leo Juni 25, 2025 umetembelea ofisi za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa lengo la kujitambulisha Wizarani pamoja na kuelezea madhumuni la kuanzisha umoja huo ambayo yanashabiana na majukumu ya wizara.
Akizungumza na ugeni huo, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt John Jingu ameupongeza uongozi wa Umoja huo kwa kuona umuhimu wa kuwa na Chombo cha kuwaongelea na ambacho kinajihusisha na kuhakikisha mtoto anapata malezi salama.
Nawapongeza kwa kujitoa kwenu kwa ajili ya jamii yetu. Wizara ipo tayari kushirikiana nanyi katika kutekeleza afua mbalimbali za ustawi wa jamii. Tunayo majukumu la kupinga ukatili wa jkijinsia, kuhamasisha jamii inaondokama na umaskini kwa kuwapa mikopo yenye gharama nafuu, na kupigav vta ongezeke lla idadi ya watoto wa mitaani, Amesema Dkt. Jingu.
Kwa upande wa Mwenyekiti i wa Umoja Wanaume, Claude Benedict ameushukuru uongozi wa wizara kwa mapokezi mazuri yenye mlengo wa kuendelea kushirikiana na kufanya kazi pamoja.
“Tupo tayari kupokea ushauri wa kitaalam ili tuwezekufikia malengo ya umoja wetu tuliyojipangia, tunaomba milango ya wizara iwe wazi kwetu hasa tunapokuwa na uhitaji wa msaada ya kitaalam, amesema Claude.