Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

DKT JINGU AWATAKA VIJANA KUCHAGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI.

Imewekwa: 30 Jun, 2025
DKT JINGU AWATAKA VIJANA KUCHAGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI.

Na WMJJWM- Dar Es Salaam

Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu amewataka vijana kuchangamkia fursa za kiuchumi zinazotolewa na Serikali ili kujiajiri na kuajiri wengine.

Dkt Jingu ameabainisha hayo June 21, 2025 mkoani Dar Es Salaam wakati akizungumza kwenye Tamasha la Vijana la Twenzetu kwa Yesu lililoandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Dkt. Jingu amesema Serikali imefungua mifuko katika nyanja mbalimbali kuwawezesha vijana nchini (Tanzania Bara) kupata mitaji kwa njia ya mikopo yenye masharti nafuu ili kuanzisha au kuendeleza miradi yao ya uzalishaji mali. Kupitia mikopo hiyo, vijana wanajitegemea, wanapunguza umaskini wa kipato na kujiajiri wenyewe.

"Vijana wa Tanzania ni nguvu kazi kubwa yenye maarifa, uwezo na ubunifu, Makadirio ya idadi ya Watu ya mwaka 2025 kwa Tanzania Bara yanaonesha kuwa idadi ya vijana wenye umri kati ya 15 - 45 ni asilimia 42.7 ya jumla ya idadi ya watu wote nchini, Takwimu hizi zinaonesha kuwa Tanzania ina nguvu kazi kubwa ya vijana ukiondoa watoto, hivyo vijana tutumie fursa zilizopo kujikwamua kiuchumi" amesema Dkt. Jingu

Amesema kukua kwa Teknolojia na ubunifu (digital innovation)
ni mojawapo ya maeneo yenye nafasi za kiuchumi kwa vijana hasa katika masuala ya ubunifu wa kiteknolojia (app ya mifumo ya biashara mtandaoni), ubunifu wa mavazi, sanaa, na filamu, ufundi wa kiufundi na utengenezaji wa bidhaa (crafts, vifaa vya majumbani),hivyo ni muhimu kujifunza na kuanzisha shughuli hizo na kujiongezea kipato.

"Kila sekta nchini ina fursa za kuwezesha vijana kujiajiri. Hivyo, kinachotakiwa ni vijana kuzifikia sekta na kutumia mitandao kujiendeleza katika kupata ujuzi utakaowawezesha kutumia fursa zilizopo kwenye sekta hizo" amesisitiza Dkt. Jingu.

Amezitaja baadhi ya fursa hizo kuwa ni pamoja na Mikopo kwa vijana ya asilimia kumi inayotolewa katika halmshauri zote nchini, Mikopo kwa wafanyabiashara ndogondogo inayotolewa na Benki ya NMB ambapo mikopo hiyo inaratibiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum