Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

AMANI NA USALAMA KWA WANAWAKE NI MUHIMU KATIKA MAENDELEO ENDELEVU YA TAIFA

Imewekwa: 20 Nov, 2026
AMANI NA USALAMA KWA WANAWAKE NI MUHIMU KATIKA MAENDELEO ENDELEVU YA TAIFA

Na WMJJWM- Morogoro

Amani na usalama kwa wanawake ni jambo muhimu linalopaswa kuzingatiwa katika kufikia maendeleo endelevu ya Taifa.

Hayo yamesemwa Novemba 19, 2026, mkoani Morogoro na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Yahaya Mmbaga wakati akizungumza na Kikosi Kazi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kinachofanya maandalizi ya taarifa za mipango kazi ya kisekta kwa ajili ya kuandaa taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama (2025–2029).

Mmbaga amesema, wanawake ni miongoni mwa makundi yanayoathirika na migogoro ya aina mbalimbali katika jamii, hivyo ni muhimu kuhakikisha migogoro inazuiliwa kuanzia ngazi ya familia, jamii hadi Taifa ili kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo bila hofu.

“Athari ya migogoro katika jamii huwafikia Wanawake zaidi, hivyo ni muhimu kuhakikisha ujenzi wa dhana ya amani na usalama kwa wanawake inapewa kipaumbele ikiwemo kuzingatiaji maoni yao katika shughuli za maendeleo ya jamii, uongozi na uchumi shirikishi.” amesema Mmbaga.

Ameeleza kwamba, lengo la maandalizi ya taarifa hiyo ni kuimarisha uratibu wa utekelezaji, ufuatiliaji wa maendeleo na utoaji wa taarifa kuhusu utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama.

Aidha, mpango kazi huo unalenga kuhakikisha wanawake na wanaume wanashiriki katika hatua zote za kuzuia na kutatua migogoro, ujenzi wa amani pamoja na masuala ya ulinzi na usalama.

Kwa upande wake, Afisa Mchambuzi wa Sera na Uratibu wa Masuala ya Amani na Usalama kwa Wanawake kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake (UN Women), Adolphina Emmanuel, amesema utekelezaji wa programu za wanawake, amani na usalama unapaswa kuleta matokeo yaliyokusudiwa na manufaa halisi kwa walengwa.

Akifafanua baadhi ya matokeo yanayotarajiwa, Adolphina amesema ni kuongeza ushiriki wa wanawake katika ngazi mbalimbali za maamuzi, hususani katika masuala yanayohusu usalama, kujenga na kuandaa viongo

slot gacor