WCF YAWEZESHA WATOTO WATOTO MAKAO YA TAIFA KIKOMBO KUPATA BIMA YA AFYA
Serikali inathamini ustawi wa watoto nchini hususan wanaoishi katika mazingira magumu.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana,Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Rahma Kisuo katika hafla ya ugawaji wa bima za afya kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ikiwa ni sehemu utekelezaji wa mpango wa kurejesha rasilimali kwa jamii (CSR), Januari 15, 2026 katika makao ya Taifa ya Kikombo yaliyopo mkoani Dodoma.
Mhe. Rahma amesema tukio hilo ni juhudi za Serikali katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wake ikiwemo watoto.
Serikali yajidhatiti kuhakikisha wafanyabiashara ndogondogo wanainuka kiuchumi kwa kuweka mazingira wezeshi na mipango madhubuti inayoimarisha uratibu na usimamizi wao nchi nzima.
Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba alipokuwa akizungumza katika Kongamano la Wamachinga, madereva pikipiki bajaji za kubeba abiria, Mama Lishe na Baba Lishe Januari 08, 2025 Jijini Dar Es Salaam.
Dkt Mwigulu amesema Serikali sikivu chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imesikia na kuzingatia hoja za wafanyabiashara ndogondogo wanazokumbana nazo na kuahidi kukaa na Wizara zinazohusika na Makundi hayo na kuweka mikakati ya kutatua changamoto hizo.
“Tutakaa pamoja na Mawaziri wa Wizara zinazowaratibu hivyo nawaomba mtoe fursa kwa Serikali kwa kushirikiana na viongozi wenu kutafakari ili tufanye jambo ambalo litawarahisishia shughuli zenu” amesema Dkt. Mwigulu.
Vilevile Dkt. Mwigulu amesema kwamba katika miaka mitano ijayo kuanzia mwaka wa fedha wa 2025/2026 Serikali itaongeza fedha ya mafungu ya vijana,wanawake na Makundi Maalum kwa ajili ya makundi hayo.
Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.Dkt Dorothy Gwajima amebainisha juhudi zilizokwisha chukuliwa na Wizara kwa kushirikiana na Wizara nyingine katika kuwainua wafanyabiashara ndogondogo toka ilipokabidhiwa jukumu ya kuwaratibu na kuwasimamia wafanyabiashara ndogondogo.
“Tulianza na programu ya kuwatambua wafanyabiashara ndogondogo kupitia mfumo wa kidigitali ambapo waliotambuliwa ni 115794 na katika kuimarisha elimu hii yamefanyika makongamano mikoa yote kasoro mmoja tu na Mikoa 21 imeshajenga Ofisi za Machinga kasoro miaka 5 ya Simiyu, Mwanza, Singida,Kigoma, Rukwa bado inaendelea na ujenzi” amesema Dkt. Gwajima
Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Wafanyabiashara ndogondogo SHIUMA Ernest Matondo ameishukuru Serikali kwa jitihida za kuwasikiliza na kuhakikisha wanainuka na kuwa na mazingira rafiki ya kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuwatengea maeneo na kuwajengea ofisi za machinga nchi nzima