Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

SERIKALI, WADAU KUSAMBAZA MKAKATI KUTOKOMEZA UKEKETAJI MIKOA VINARA

Imewekwa: 20 Jul, 2026
SERIKALI, WADAU KUSAMBAZA MKAKATI KUTOKOMEZA UKEKETAJI MIKOA VINARA

Na WMJJWM, Dodoma

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na Shirika la C-Sema kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya imeanza kusambaza Mkakati wa Kitaifa wa Kisekta wa Kutokomeza Ukeketaji (mwaka) kwenye mikoa inayoongoza kwa ukeketaji.

Kampeni hiyo inayojulikana kama karavani ya kusambaza Mkakati wa Taifa wa Kisekta wa Kutokomeza Ukeketaji inafanyika katika mikoa mitano ya Dodoma, Manyara, Arusha, Mara na Singida kuanzia Julai 19, 2026.

Akizindua msafara huo Julai 19, 2026 jijini Dodoma, Mzee wa Mila, Chifu Mazengo wa pili mkoa wa Dodoma amewataka wananchi kuachana na mila hiyo ya ukeketaji kwani inakiuka misingi ya haki za binadamu.

“Mila zetu ziwe chachu ya maendeleo badala ya chachu ya matatizo, sisi machifu tunasisitiza kumlinda mtoto wa kike na tunaunga mkono utekelezaji wa mkakati huu." amesema Chifu Mazengo.

Mratibu wa msafara wa kusambaza mkakati huo, Dennis Moses amesema msafara huo unaongozwa na Kaulimbiu isemayo “Ukeketaji ni Kinyume cha Sheria na Haki za Binadamu; Chukua Hatua." inayoakisi dhamira ya pamoja na uwajibikaji wa jamii katika kutokomeza ukeketaji nchini. 

“Ukeketaji si jukumu la Serikali pekee, bali ni wajibu wa kila mwanajamii, wakiwemo wazazi, viongozi wa dini, viongozi wa kimila, vijana, wanawake, wanaume, walimu, watoa huduma, vyombo vya habari na wadau wa maendeleo”. amesisitiza Dennis.

Aidha, amefafanua sababu ya Mkakati huo kusambazwa kwenye mikoa hiyo ni kutokana na kushamiri kwa vitendo hivyo akitaja mkoa wa Arusha na Manyara kuongoza kwa asilimia 43.

Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, wanapita katika Halmashauri sita  kusambaza mkakati huo ikiwemo Chemba, mkoani Dodoma na wataendelea katika Halmashauri za Monduli, Babati, Serengeti, Tarime na Singida.

slot gacor