SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII- WAKILI MPANJU

SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA VYUO VYA MAENDELEO YA JAMII- WAKILI MPANJU
📌AZINDUA JENGO LA UTAWALA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII MLALE – SONGEA
Na Abdala Sifi – Ruvuma
Â
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuboresha miundombinu na mazingira rafiki kwa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vinavyosimamiwa na Wizara Â
ili wanafunzi waweze kupata elimu yenye tija kwa maendeleo ya jamii.Â
Wakili Mpanju ameyasema hayo leo tarehe 02 Oktoba, 2025 wakati akizindua jengo la Utawala la Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale kilichopo Kata ya  Magabura wilayani Songea mkoani Ruvuma.
“Napenda kuwahakikishia kwamba kipaumbele cha Wizara ni kuendelea kujenga majengo mapya na kukarabati yaliyopo ili kukifanya Chuo hiki kutoa mafunzo bora na kimbilio  kwa vijana wetu kutoka mikoa jirani kama vile Lindi, Mtwara na Njombe kuja kupata elimu hapa kwa maendeleo endelevu katika jamii yetu” amesema Wakili Mpanju.Â
Aidha Wakili Mpanju amewapongeza watumishi wa Chuo hicho na kuwasisitiza kujiendeleza kielimu na ujuzi mbalimbali ili kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia, ili waweze kuwafundisha wanafunzi kwa tija.Â
Naye Mkuu wa hicho Luciana Mvula amesema ujenzi wa jengo hilo umesaidia kuziba pengo  la ofisi za watumishi na kuahidi kwa uongozi wa Chuo utahakikisha jengo hilo linatunzwa kwa maslahi ya vizazi vijavyo.
Aidha Luciana amesema Chuo kitaendelea kuzalisha Maafisa Maendeleo ya Jamii ambao ndiyo nyenzo ya kubadili mitazamo chanya kwa jamii ili kupokea mabadiliko mbalimbali ya kimaendeleo. Â
MWISHO