Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

RAIS SAMIA ATOA MKONO WA EID KWA WENYE UHITAJI, WAZIRI GWAJIMA AMUWAKILISHA

Imewekwa: 31 Mar, 2025
RAIS SAMIA ATOA MKONO WA EID KWA WENYE UHITAJI, WAZIRI GWAJIMA AMUWAKILISHA

Na WMJJWM - Dar Es Salaam.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Mheshimiwa Dkt Dorothy Gwajima ametoa wito kwa Jamii kuwapenda, kuwajali na kuwahudumia Makundi ya wenye mahitaji Maalum ili kukuza Umoja na mshikamano katika Jamii.

Dkt Gwajima amesema hayo Machi 28, 2025, akiwa amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa utaratibu wa utoaji zawadi za sikukuu mbalimbali ambapo msimu huu ni kuelekea Id El Fitri  na Pasaka ambapo, Zawadi hizo zimeenda kwa watoto, wazee na watu wenye ulemavu katika vituo 24 ambapo kati ya hivyo 5 ni vya Zanzibar.  

Katika zoezi hilo walioungana na Serikali ni pamoja na Wadau wa Maendeleo, Taasisi na  Mashirika  yanayohudumia watu wenye Mahitaji Maalum ambapo, tukio hilo limefanyika katika Makao ya  Taifa ya Watoto Yatima, Kurasini Jijini Dar Es  Salaam.

" Nitoe wito kwa Jamii kuwa, kila mmoja ana wajibu wa kuwahudumia watoto na watu wenye mahitaji maalum, siyo tu kwa siku za sikukuu, bali ni kwa muda wote ili kuwapa faraja na huo ndio upendo tunaotakiwa kuwaonesha"

Zawadi hizo ni muendelezo wa utaratibu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan, kuwakumbuka watu wenye mahitaji maalum Ili, nao waweze kuungana na wengine wote kufurahi katika nyakati za sikukuu kama vile Christimas, Mwaka  Mpya, Idd na Pasaka.

Miongoni mwa zawadi hizo ni vyakula, viburudisho, viifaa vya shule, Majiko, Mashine za kufulia, Majokofu na vitendea kazi mbalimbali ambapo, katika kipindi cha mwaka 2024/25 jumla ya Vituo 153 Tanzania Bara na Zanzibar vimenufaika kwa  zawadi hizo, lengo la likiwa ni kuwaendeleza watoto na kuimarisha utoaji wa huduma katika  Makao ya Watoto.

Kwa upande wake Kamishna msaidizi wa idara ya ustawi wa Jamii katika  Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Tullo Masanja amesema, ili kuwa na ustawi wa maisha ya kijamii ni lazima kumjali kila mtu kwa kumsaidia na kumpa msaada ili aweze kukidhi mahitaji muhimu ya kila siku.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Amani Foundation for Orphanage, Hijjat Zubeida, akizungumza baada ya kupokea zawadi hizo amempongeza Rais Samia Kwa moyo wa upendo na kuwajali watu wenye mahitaji Maalum huku akitoa wito wa Wadau mbalimbali kujitolea ili kuendelezwa moyo wa upendo na faraja Kwa Makundi hayo.