Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

MAAFISA MAENDELEO IBUENI  FURSA KWA JAMII-FELISTER MDEMU.

Imewekwa: 18 Oct, 2025
MAAFISA MAENDELEO IBUENI  FURSA KWA JAMII-FELISTER MDEMU.

MAAFISA MAENDELEO IBUENI  FURSA KWA JAMII-FELISTER MDEMU.

Na Witness Masalu- Iringa

Naibu Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii Felister Mdemu ametoa amewahimiza  maafisa Maendeleo ya Jamii nchini kuubua fursa za maendeleo katika jamii zao na kuwajengea uwezo wananchi kuhusu namna ya kunufaika na fura hizo.

Mdemu amebainisha hayo Oktoba 17,2025 Mkoani Iringa alipotembelea na kukagua uendeshaji wa miradi katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rungemba.

Felister amesema wataalam  wa Maendeleo ya Jamii wanatakiwa kwenda mbali zaidi ya kutoa hamasa  peke yake kwa wananchi bali wanatakiwa kuhakikisha wanawejengea uwezo wa kuweza kunufaika kupitia fursa wanazoibainisha

“Wataalam  kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rugemba wamewahamasisha wananchi kushiriki katika kilimo cha parachichi pamoja na kuwalea katika kila hatua ili waweze kunufaika na juhudi zao na kujipatia maendeleo”amesema Felister

Vilevile Felister amewapongeza wataalam wa Maendeleo ya Jamii kutoka chuo hicho kwa kutatua changamoto ya lishe katika Mkoa iringa kupitia ubunifu .

“Pamoja na Mkoa huu kulima mazao mengi lakini bado kulikia na changamoto ya lishe  hivyo Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kutoka Chuo cha Maendeleo Ya Jamii-Rugemba waliweza kubaini mbinu za kuelimisha jamii ili waweze kuondokana na tatizo hilo”amesema Felister.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii Patrick Golwike amesema chuo hicho kinazidi kutanua wigo wake kwa  kuboresha mitaala ili kutimiza dhumuni lake ambalo ni kutoa wataalam wenye weledi wa kuhudumia jamii na kuleta fursa zenye manufaa.

“Uboreshaji wa Mitaala umekuwa ukifanyika kila baada ya muda kupitia ushirikiano wa taasisi za Maendeleo ya Jamii kupitia kujengeana uwezo na kubadilishana maarifa kwani kila taasisi ina cha kujifunza kutoka kwa taasisi nyingine”amesema Golwike.

Naye mmoja wa wanufaika wa usimamizi wa miradi unaotekelezwa na  Chuo cha Maendeleo ya Jamii-Rugemba Kelvin Mwaihojo  ameishukuru serikali kupitia chuo hicho kwa kuwekeza juhudi zake na kuwaletea wataalam walioweza kuwatambulisha katika fursa za kiuchumi na kuwasimamia katika kila hatua mpaka kufikia mafanikio makubwa.


Mwisho.