KATAVI YAPATIWA MAFUNZO YA MWONGONZO WA MADAWATI YA JINSIA KUKABILI UKATILI SOKONI

Na WMJJWM, Katavi.
Serikali yaendelea kuzindua madawati ya kupinga ukatili wa kijinsia Katika maeneo ya umma, hasa katika masoko ili kupunguza Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ambavyo vimekuwa vikijitokeza kwa wanawake na watoto.
Hayo yamebainishwa leo tarehe 10 Februari 2025 na Katibu tawala msaidizi Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa mkoa wa Katavi Florence Lungwa wakati anafungua mafunzo ya mwongozo wa Uanzishwaji na uendeshwaji wa dawati la kutokomeza vitendo vya ukatili wa Kijinsia katika maeneo ya Umma Mkoani Katavi.
“Maeneo haya yamekuwa na malalamiko mengi ya vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ikiwa ni pamoja na lugha chafu za udhalilishaji, miundombinu mibovu ya utendaji kazi, kukosekana kwa Usawa wa ushiriki wa Wanawake kwenye nafasi za Uongozi na maamuzi, kutokuwa na mazingira salama ya watoto wanaofika kwenye hayo pamoja na kukosekana kwa madawati ya Kijinsia yanayoweza kusaidia wahanga wanaofanyiwa vitendo vya Ukatili wa Kijinsia.”amesema Lungwa.
Amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira salama katika jamii kupitia utekelezaji wa afua mbalimbali ili kupunguza Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ambavyo vimekuwa vikijitokeza hasa kwa wanawake na watoto.
Aidha, Lungwa amefafanua ameeleza kwamba Mwongozo huu utawezesha kuanzishwa kwa madawati hayo ambayo yatakuwa ni muarobaini wa kushughulikia masuala ya Ukatili wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake kwenye maeneo yaliyolenga.
Mafunzo hayo ni mahsusi kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, na Masoko, wa Mkoa na Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi. Pia yamejuuisha Wenyeviti wa Masoko, Afisa Dawati anayeshughulikia masuala ya Ukatili wa Kijinsia Polisi pamoja na Wawakilishi ngazi ya, kutoa Shirikisho la Umoja wa Machinga (SHIUMA) ngazi ya Mkoa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Jinsia Rennie Gondwe ameeleza kwamba kutokana na tafiti zilizofanywa mwaka 2019 na serikali kupitia Shirika la Equality for Growth ulibaini kuwa maeneo ya masoko yamekuwa na matukio mengi ya Ukatili wa Kijinsia hususan kwa Wanawake na Watoto