ELIMU YA FEDHA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE NI MUHIMU KWA MIRADI YAO - MDEMU
ELIMU YA FEDHA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE NI MUHIMU KWA MIRADI YAO - MDEMU
Na Abdala Sifi - WMJJWM- Singida
Ili kuongeza tija katika kuinua shughuli za vikundi vya Wanawake wajasiriamali ni muhimu kuendelea kuwapa elimu ya fedha kwa ustawi wa shughuli zao.
Hayo yamebainishwa leo tarehe 17 Desemba 2025, na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Felister Mdemu akizingumza na Wanawake wanufaika wa mkopo unaotolewa na Wizara hiyo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF).
Mdemu amefanya ziara hiyo katika Kata ya Matongo, Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida kwa lengo la kupata taarifa za utekelezaji wa miradi yao na namna wanavyoinuka kiuchumi kupitia mikopo hiyo.
"Niwaombe Maafisa Maendeleo ya Jamii, kila mnapoandaa makomgamano, vikao na matunzo mbalimbali nii muhimu sana kupata kuwalika wataalamu kutoka katika Taasisi za fedha ili wawezea kutoa elimu ya fedha kwa Wanawake ili wakuze mitaji na kuweka akiba na kuendesha miradi yao bila hasara" amesema Mdemu.
Aidha Naibu Katibu Mkuu Mdemu amewataka Wanawake kupendana na kushirikisha wengine kuhusu fursa mbalimbali za kiuchumi ili kwa pamoja waweze kujiletea Maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mtendaji wa Wilaya ya Mkalama Seleman Musungu amesema Wanawake wanaendelea kuchangamkia fursa za mikopo mbalimbali inayotolewa na Serikali ambapo inawawezesha kuendesha miradi ya maendeleo na kukuza uchumi wa Kaya.
Nao miongoni mwa Wanawake walionufaika na mkopo wa Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake Aida Abdallah ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwezesha Wanawake kiuchumi huku akiomba kupatiwa mkopo awamu nyingine baada ya kikundi chake kukamilisha marejesho ya mkopo wa awali jumla ya shilingi milioni ishirini.
MWISHO