Matangazo

Imewekwa: Feb 01, 2022

TANGAZO KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs)

TANGAZO KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI (NGOs)

Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) anayatangazia Mashirika yaliyosajiliwa na yanayofanya shughuli zao katika Mikoa ya Dodoma, Singida na Iringa kwamba, Wizara itafanya kikao na viongozi wa Mashirika hayo Mkoani Dodoma. Kikao hicho kitafanyika tarehe 05 Februari, 2022 kuanzia 2.30 asubuhi kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Lengo la kikao hicho ni kuzungumzia masuala ya utendaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na nafasi yao katika kushirikiana na Serikali kutatua changamoto mbalimbali katika Jamii.

Aidha, Ofisi ya Msajili itaendesha zoezi la uhakiki na kubadili vyeti vya zamani vya NGOs na kutoa vyeti vipya vyenye ukomo wa miaka kumi (10) kwa NGOs zilizosajiliwa katika Mkoa wa Dodoma, Singida na Iringa kulingana na Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 (Sura 56) kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 3 ya mwaka 2019. Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa - Dodoma kuanzia tarehe 05 hadi 11 Februari, 2022 (saa 2.30 asubuhi hadi saa 11.00 jioni).

Ili kufanikisha zoezi hilo, Kiongozi au Mwanachama wa NGO anapaswa kufika na nyaraka zifuatazo:

(i)Cheti halisi (Original) na nakala ya cheti hicho.

(ii)Orodha ya Wanachama na saini zao;

(iii)Wasifu (Curriculam Vitae) wa viongozi watatu wa Shirika pamoja na Namba ya kitambulisho cha Taifa (NIDA)-kwa Wanzania na nakala ya pasi ya kusafiria (Passport) kwa raia wa kigeni;

(iv)Katiba iliyogongwa mhuri wa Ofisi ya Msajili;

(v)Nakala ya risiti ya malipo ya ada ya mwaka (annual subscription fees) kwa mwaka 2018, 2019, 2020 na 2021.

(vi)Muhtasari wa wanachama uliopitishwa kama/endapo kuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika hivi karibuni.

Vickness G. Mayao

MSAJILI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

Simu: 0737 569 583/ 0737 569 584