Matangazo

Imewekwa: Dec 21, 2022

TAARIFA MUHIMU

Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali anayatangazia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) kuwasilisha taarifa zao za mwaka 2022 na kulipa ada kuanzia tarehe 01 Januari, 2022. Ada ya mwaka ni Shilingi 50,000/= kwa Mashirika ya Ndani (Local NGOs) na USD 100 kwa Mashirika ya Kimataifa (International NGOs). Mwisho wa kuwasilisha taarifa na kulipa ada ya mwaka 2022 ni tarehe 15.4.2022 saa 6: 00 Usiku. Baada ya tarehe hiyo malipo yote ya ada yatalipwa na faini ya TShs.100,000/= kwa Mashirika ya Ndani (Local NGOs) na USD 300 kwa Mashirika ya Kimataifa (International NGOs).

Taarifa hizo ziwasilishwe kupitia mfumo wa usajili wa NGOs (nis.jamii.go.tz) kwa kutumia akaunti za Mashirika. Aidha, kwa wale wasio na Akaunti kwenye mfumo waombe kupitia jamii.go.tz katika kipengele cha NGOs MIS na kisha kujaza fomu kiufasaha na kuiwasilisha kwenye mfumo. Hautatolewa muda wa ziada wa kuwasilisha taarifa, na kutowasilisha taarifa ni kinyume na kifungu cha 29(1) (a) na (b) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na.24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005 na 2019.

MSAJILI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI Tel: 0737 569 583/ 0737 569 584/0762 361 646 12 Disemba, 2022 _____________